The House of Favourite Newspapers

Fei Toto, Dube Wapewa Kazi Maalum Azam

0

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Yousouph Dabo, amesema kikubwa ambacho wachezaji wake wanatakiwa kukifanya ikiwa ni pamoja na kiungo Feisal Salum na mshambuliaji Prince Dube ni kujitoa muda wote kutafuta ushindi.

Dabo ambaye ameiongoza Azam kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu na kushinda zote, amesema: “Kwa namna ambavyo tunafanya maadalizi kwa mechi zijazo ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa kujitoa zaidi ili kupata matokeo mazuri uwanjani.

“Tunaamini kuna makosa ambayo yanatokea, hayo tunayafanyia kazi ili kuwa imara kwa mechi zijazo. Ushindani ni mkubwa, hilo lipo wazo nasi tunajitahidi kufanya kazi nzuri kupata matokeo,” alisema Dabo.

Mchezo ujao kwenye Ligi Kuu Bara, Azam FC inatarajiwa kucheza Septemba 21, mwaka huu dhidi ya Singida Fountain Gate.

RAIS SAMIA KWENYE ZIARA ya KIKAZI MTWARA, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KWENYE MKUTANONI…

Leave A Reply