The House of Favourite Newspapers

Fei Toto, Mayele Wala Kiapo Kuifunga Namungo

0

MASTAA wa Yanga ni kama wamekula kiapo kuhakikisha leo Jumamosi wanaibuka na ushindi dhidi ya Namungo kutokana na kuweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu dhidi ya wapinzani
wao.


Yanga leo watakuwa
ugenini mkoani Lindi kumenyana na Namungo katika mchezo wa mzunguko wa sita wa ligi kuu ambapo mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Ilulu uliopo mkoani humo.


Katika ligi hiyo Yanga
kwa sasa ndio vinara wa ligi wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 15 mara baada ya kufanikiwa kushinda michezo yake yote waliyocheza.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alisema kuwa malengo yao ni kuendeleza ushindi ambao wameupata katika michezo mitano iliyopita huku mshambuliaji Fiston Mayele yeye akisema kuwa kila mchezo kwao wanauchukulia kama fainali, hivyo watapambana kwa ajili ya kuondoka na ushindi.

 

“Tumeshinda michezo yetu mitano ya mwanzo wa ligi, hakuna ambaye anasema sasa inatosha mpaka pale tutakapoona kuwa tumetimiza malengo yetu.

 

“Kila mtu anafahamu kuwa Yanga msimu huu tunahitaji ubingwa, hivyo hatutakubali kuona tunapoteza mchezo wowote uliopo mbele yetu,” alisema Feisal.

 

Mayele alisema: “Kila mchezo kwetu tunauona kama ni fainali, hakuna ambaye hafahamu timu huwa zinacheza vipi katika mechi za fainali, huwa zinapambana sana, basi na sisi tupo hivyo yote ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa msimu huu.

STORI NA MARCO MZUMBE, CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply