The House of Favourite Newspapers

Feisal Ashinda Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Novemba 2023 Wa Ligi Kuu

0
Kiungo wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal Salum.

Kiungo wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Feisal Salum, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba 2023 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara akiwapiku Maxi Nzengeli wa Yanga na Kipre Jr. wa Azam FC.

Taarifa ya Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya jana Desemba 5, imemtangaza kocha wa Azam FC, Bruno Ferry kuwa kocha bora wa mwezi huo akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga na Heron Ricardo wa Singida Fountain Gate.

Aidha meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga, Nassor Makau amechaguliwa kuwa Meneja bora wa uwanja kwa mwezi Novemba 2023.

KUTOKA GHANA: ALI KAMWE AFUNGUKA KABLA ya KUIVAA MEDEAMA – “MKIMPIGA AHMED ALLY MTAMUUA”…

Leave A Reply