Ferdinand: De Gea Ataondoka Man U

MKONGWE wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema kitendo cha kipa David De Gea kuwekwa benchi ni wazi staa huyo hataendelea kusalia ndani ya kikosi hicho.

 

Hii ni baada ya De Gea kuwekwa benchi hivi karibuni katika mchezo wa Premier League dhidi ya Brighton wakati Man United ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 

Kocha Ole Gunnar Soskjaer hivi karibuni amenukuliwa akisema kuwa anapata mtihani kuwa kuchagua kati ya De Ge ana Dean Henderson atakuwa kipa namba moja.

 

“Kwenye soka unaweza kuwa na nafasi mbili ya kuchagua kwamba kuwania nafasi yako au kuamua kuondoka kuangalia sehemu nyingine.

 

“Kama Dean Henderson atamaliza msimu huu akitumika kama kipa namba moja, lakini siyo De Gea anaendelea kubaki Man United kwa hali hiyo anaweza kuondoka.

 

“Mshahara wake ni mkubwa lakini hiyo haijalishi mwisho wa siku kama huna nafasi ndani ya timu inakuwa haina maana.

“De Gea anaweza kubaki ndani ya timu au Ole anaweza kuona mambo tofauti.

 

Kwa sasa anamuweka Henderson mbele, lakini De Gea atakubali hali hiyo na kuendelea kukaa hapo.“Henderson ametafuta nafasi kwa muda mrefu sasa amepata, lakini pia Ole ameona kitu ndani yake ndiyo maana ameamua kumpa nafasi sasa kuweza kukionyesha, De Gea atamsapoti, ila ataumia moyoni.

Toa comment