The House of Favourite Newspapers

FEROOZ AANIKA KILICHOMFELISHA KWENYE GAME

Feruzi Mrisho Rehani ‘Ferooz’

KWA wapenda muziki mzuri wenye ujumbe bila shaka watakuwa na kumbukumbu nzuri za ‘nyimbo za taifa’ kama Bosi au Starehe? Kama hiyo haitoshi, watakumbuka pia wimbo wa majonzi wa Kamanda ambao waliufanya kama Kundi la Daz Nundaz, humo ndani, sauti ya kichwa kinachokwenda kwa jina la Feruzi Mrisho Rehani ‘Ferooz’ kilikonga nyoyo vilivyo.  

 

Jamaa alifanya makubwa sana kiasi cha kumgusa rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa ambaye ilisemekana alimpa zawadi ya ndinga la kifahari aina ya Jeep baada ya wimbo wake wa Sterehe kufanya vizuri na kufikisha ujumbe kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi.

Hapa katikati mchizi alikuwa kimya kidogo kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Showbiz Xtra imemtafuta na kupiga naye stori, twende tukamsikie:

 

Showbiz Xtra: Ferooz mbona uko kimya sana nini kimekusibu kwenye muziki?

Ferooz: Nipo napambana maana game ya muziki ni kama maisha mengine ambayo ni mzunguko unaweza ukawa juu au ukashuka. Napambana kupanda juu upya.

Showbiz Xtra: Hebu wakumbushe mashabiki wako, hivi ule Wimbo wa Bosi ulikuwa ni kisa cha kweli au vipi?

 

Ferooz: Naweza nikasema ni cha kweli lakini siyo kama kimenitokea mimi, kwa kuwa ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii nikajiuliza tu kwa nini nisitoe wimbo maana mabosi wengi huwa wanafanya vile ni vitu ambavyo vipo na mpaka sasa vipo na vinahitajika kukemewa.

Showbiz Xtra: Ukimya wako unatia shaka kidogo au ndio umeshaachana kabisa na muziki?

Ferooz: Sijaachana na muziki na siwezi kwa sababu muziki ndio maisha yangu ila ni changamoto tu zilinipitia ndio maana nikawa kimya?

 

Showbiz Xtra: Umesema hujaacha muziki je, kitu gani unakifanya ili kuwaaminisha mashabiki wako kwamba hujaacha muziki?

Showbiz Xtra: Kuna ngoma nimerekodi kwa Produza P Funk anamaliziamalizia mixing na nyingine nafanya kwa Moko Ginius. Nimeshamalizia nyimbo mbili ambazo ni Nakaza Roho na Najaribu.

Showbiz Xtra: Kwa hiyo utakuwa mwenyewe au na Kundi la Daz Nundaz?

Ferooz: Hapana nipo peke yangu kwa kuwa wenzangu hawapo, tuligaw-anyika kwa sababu mkishakuwa timu kila mtu anakuwa na maamuzi yake basi ikawa ni biashara kila mtu anataka maslahi ikabidi tugawanyike na makundi mengi yaligawa-nyika kwa mfano Hard Blastaz, East Coast siyo sisi tu.

Image result for FEROOZ

Showbiz Xtra: Sasa hivi muziki umekuwa na upinzani mkubwa umejipangaje kupambana?

Ferooz: Mimi naamini muziki wangu upo palepale nina mashibiki wangu bado wananiamini na wanaendelea kuupenda muziki wangu najua kila mtu ana muziki wake na staili yake kwa hiyo naamini nitafanya vizuri na watanipokea kwa kile ambacho ninacho kwenye sanaa.

Showbiz Xtra: Kipindi cha nyuma mlikuwa mnatoa audio na baadaye ndio mnatengeneza video sasa mambo yamebadilika watu wanatoa vyote kwa pamoja, umejipanga vipi maana lazima gharama ziongezeke.

 

Ferooz: Yah hiyo ni changamoto lakini nashukuru nimeweza kupambana nayo kwa sababu nyimbo ambazo nitazitoa mwezi ujao Mungu akipenda zitakuwa moja kwa moja na video.

Showbiz Xtra: Inasemakana kuvurugika kwenye kundi lenu moja ya sababu ni matumizi ya madawa ya kulevya unalizungumziaje hilo?

 

Ferooz: Hapana hatukujiingiza kwenye madawa ya kulevya kwa sababu kuna vitu ambavyo vinatokea kwenye kundi kama migogoro mara huyu anasema hivi, mara vile nikaamua kuhama kwenye menejimenti kuna kipindi nilikuwa kwa Mkubwa Fela, unajua mkishaanza migogoro lazima mshuke kwenye kazi mkiwa kundi na kikubwa ni kwenye mgawanyo wa fedha ndio ilikuwa shida na si kweli kwamba madawa ya kulevya ndio yaliua kundi ni maneno tu ya watu wakiona unashuka wanazungumza yao lakini mimi nipo safi ukiniangalia na hata sauti yangu pia iko safi.

 

Showbiz Xtra: Ni nyimbo gani ambazo mpaka leo huwa unazikumbuka na zilifanya vizuri?

Ferooz: Nyimbo ambazo zilibamba na huwa najisikia vizuri sana zinapopigwa kwenye media bado ni Kamanda, Bosi, Nipe Tano, Barua na nyingine nyingi.

Showbiz Xtra: Mafanikio yapi uliyoyapata kupitia muziki?

Ferooz: Mafanikio niliyoyapa kwanza namshuru Mungu kwa kuwa ninafahamika, nimejenga jina mpaka nimekuwa Ferooz ambaye najulikana nina mashabiki wengi na ndio kikubwa ambacho msanii yeyote anachokihitaji.

 

Showbiz Xtra: Unamuelezeaje marehemu Mangwea, alikuwa ni mtu wa aina gani kwako?

Ferooz: Mangwair alikuwa ni mtu wa furaha tu alikuwa hana bifu na muda wote alikuwa ni mtu wa kuimbaimba yaani alikuwa anapenda sana muziki.

Showbiz Xtra: Una biashara gani tofauti na muziki?

 

Ferooz: Dah! Kwa sasa sina biashara, kuna biashara ambayo nilijaribu kuifanya ya madini kiukweli ilinipotezea pesa nyingi sana karibu milioni 100 lakini nilipoteza tu sikuwa na bahati nayo na ilinifanya niyumbe kwa sababu nilipoteza hela nyingi nikawa na mawazo nafikiri na hicho kilisababisha kushuka kwangu lakini namuomba Mwenyezi Mungu anisimamie kwa sasa nifanye vizuri.

Showbiz Xtra: Unawaambia nini mashabiki wa Ferooz?

Ferooz: Mashabiki wangu wasikate tamaa nipo na sasa narudi kama zamani mwezi ujao!

STORI: NEEMA ADRIAN

Comments are closed.