The House of Favourite Newspapers

FEZA KESSY APIGA CHINI UTANGAZAJI , AMFUNGUKIA MWANAYE

Tokeo la picha la FEZA KESSY
FEZA KESSY

FEZA Kessy aka Manzi ya Arusha ni miongoni mwa mastaa ambao wamepata nafasi ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya Bongo. Alianza kufahamika zaidi mwaka 2013 akiwa ndani ya Jumba la Big Brother na ngoma yake ya kwanza kabisa kwenye muziki ni Amani ya Moyo.

Mbali na kazi hiyo ana mchango mkubwa kwenye muziki kwa kuachia kazi mbalimbali na hivi karibuni ameachia wimbo uitwao Simple, aliomshirikisha Dammy Krane, wimbo ambao unafanya vizuri kwenye media mbalimbali Bongo.

Hata hivyo mbali na kufanya vizuri kwenye muziki, Feza amejipatia jina akiwa mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Choice FM. Ijumaa Showbiz, imeamua kumtafuta na kuzungumza naye mengi kuhusu muziki. Huyu hapa;

SHOWBIZ: Feza hongera kwa kazi nzuri, vipi kuhusu mapokeo ya kazi yako mpya?

FEZA: Mapokeo kiukweli ni makubwa. Ni zaidi ya mategemeo yalivyokuwa.

SHOWBIZ: Unawezaje kumudu kuwa mtangazaji na kufanya muziki hasa unapopata shoo zinazoku-lazimu kusafiri?

FEZA: Kiukweli ni ngumu sana kufanya muziki ukiwa pia mtangazaji. Ilikuwa inanighalimu, lakini kwa sasa nimeamua kupiga chini utangazaji na kudili na muziki kwa kiasi kikubwa.

SHOWBIZ: Lakini kipi unapenda zaidi kati ya kutangaza na kufanya muziki?

FEZA: Napenda vyote. Lakini muziki upo kwenye damu zaidi.

SHOWBIZ: Unafikiri kwenye muziki nani ni mshindani wako Bongo?

FEZA: Si Bongo tu, lakini duniani kote, Feza anashindana mwenyewe. Hakuna ninayeshindana naye zaidi.

SHOWBIZ: Ni nyimbo gani ambazo unasikiliza sana kwa sasa?

FEZA: Ninasikiliza nyimbo nyingi za regge na dance.

SHOW-BIZ: Ni mwana-muziki gani Bongo unapenda kufanya naye kazi?

FEZA: Wengi sana wapo ninapenda kufanya nao kazi. Ni suala la muda tu, nitafanya kazi na wanamuziki wengi.

SHOWBIZ: Wanamuziki wengi wanafanya kolabo za nje ili kutanua wigo wao wa mashabiki vipi kwa upande wako?

FEZA: Kolabo ni jambo la msingi sana. Kama nilivyosema ni suala zima la muda. Muda ukifika kolabo za nje na sehemu mbalimbali zitafanyika.

SHOWBIZ: Umekwishawahi kukata tamaa kwenye muziki?

FEZA: Siyo kukata tamaa. Labda kuchoka tu kwa sababu wakati mwingine matokeo yanakuwa ni tofauti na nguvu ninayowekeza. Inauma sana lakini kila nikifikia wakati huo ninajikumbusha ni wapi nilipotoka na wapi nilipofika kwa sasa.

SHOWBIZ: Wanamuziki wengi wanafanya albamu, vipi kwa upande wako?

FEZA: Kwa upande wangu bado kwa sasa. Lakini mipango ipo, pengine mwakani mambo yakienda vizuri nitafanya albamu.

SHOWBIZ: Mbali na muziki na kutangaza pengine kuna ishu nyingine unafanya?

FEZA: Hapana kwa sasa. Nimepumzika kwenye biashara zangu ndogondogo lakini muda si mrefu nitawafahamisha mashabiki zangu nina mishemishe gani nyingine.

SHOWBIZ: Mwaka huu baada ya Valentine ulidai kwamba umeachwa na upo kwenye maumivu, vipi kwa sasa upo kwenye uhusiano na unadate na nani?

FEZA: Nipo kwenye uhusiano lakini ni wa siri kidogo. Kwa sasa siwezi kuweka mambo hadharani.

SHOWBIZ: Vipi kuhusu ndoa?

FEZA: Ha! Ha! Haa! Wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi na kila mtu atafahamu.

SHOWBIZ: Una mtoto wa kiume aitwaye Jay, unawezaje kumlea kama ‘single mother’ huku upo ‘busy’ na mishe za muziki?

FEZA: Ninapata muda wa kumlea mwanangu lakini ninapokuwa sipo mama yangu anakuwepo kwa ajili yangu. Nipo ninapambana Mungu akisaidia nikafikia mafanikio yangu nitafurahia maisha zaidi na mwanangu.

SHOWBIZ: Una kipi cha mwisho kwa mashabiki wako?

FEZA: Bila wao mimi si kitu. Wazidi kunisapoti na kusapoti kazi za nyumbani.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.