The House of Favourite Newspapers

Filamu Zapukutisha Hela za Vai wa Ukweli

0

MSANII wa filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiandaa kazi kwa fedha zake mwenyewe, hivi sasa hana kitu kwani licha ya kutumia gharama kubwa kutengeneza filamu, anachopata ni kidogo kiasi kwamba hajui afanye nini.

Akistorisha na Za Motomoto News, Vai alisema anatumia gharama nyingi kwenye maandalizi, lakini anapokuja kuuza kazi, fedha anazopata ni ndogo zaidi jambo ambalo limempa hasara na mpaka sasa hajui mtaji uliishia wapi.

“Sihongi na sijawahi kumuhonga mwanaume useme labda ndipo nilipomalizia mtaji, la hasha! Nilishangaa tu fedha zimeyeyuka na sina uwezo wa kutengeneza tena filamu zangu mwenyewe, niko tu nasubiri nishirikishwe za watu wengine maana kila siku maisha yanaendelea kuwa magumu jamani,” alisema Vai.

Stori: Gladness Mallya | Risasi Mchanganyiko | Za Motomoto News

Leave A Reply