FIRST CLASS YA AMIGO KUZINDUA ‘MAMA WA HIYARI’ – VIDEO

Amigo akionesha CD ya albamu hiyo (kulia) ambayo itakuwa ikiuzwa katika uzinduzi huo.

Kundi la First Class Modern Taarab leo Alhamisi, Novemba 8, 2018 limetangaza onesho la uzinduzi wa albamu yao iitwayo Mama wa Hiyari ambao utafanyika Ukumbi wa Hotel Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Akiwasisitiza jambo wanahabari.

Akizungumza na wanahabari, kiongozi wa kundi hilo Aboubakar Soud almaarufu Amigo Au Mfalme alisema uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo sita unatarajiwa kuwa wa aina yake kwa jinsi maandalizi waliyoyafanya.

Msemaji wa kundi hilo, Dokta Kumbuka Mzaramo akiongea kwa mbwembwe na wanahabari (hawapo pichani).

Amigo amesema muziki wa Taarab kwa siku za hivi karibuni ni kama ulipoteza mwelekea tangu aliyekuwa Mfalme wa muziki huo, Mzee wa Yusuf aliyekuwa akiliongoza kundi la Jahazi kuachana nao na kumrudia muumba wake lakini yeye amepania kuurudisha kwa kasi.

Wanahabari wakiwa kazini.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Muziki, na Mpiga Solo wa bendi hiyo Emeraa Solo naye akiwahakikishia wanahabari kuwa idara yake itahakikisha ‘saundi’ ya kundi hilo inakuwa na kiwango cha kimataifa.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Toa comment