Kartra

Fiston Atangaza Kushusha Mvua ya Mabao Yanga

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razack, amesema kwa sasa mashabiki wa timu hiyo wakae mkao wa furaha kwani mvua ya mabao inakuja kutoka kwake.

 

Kauli hiyo ameitoa baada ya kufungua akaunti yake ya mabao ndani ya kikosi hicho katika mchezo wa Kombe la FA uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar, Jumamsoi iliyopita dhidi ya Kengold ambapo Yanga ilishinda 1-0.

Mrundi huyu aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la FA ambapo amefanikiwa kufunga bao moja tu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Fiston amesema: “Nimefurahi kufunga bao langu la kwanza tangu kujiunga na Yanga, huu ni mwanzo, mazuri mengi yanakuja mbele kwani nimejipanga kufunga katika kila mechi.”


Toa comment