testiingg
The House of Favourite Newspapers

Fiston Mayele Achaguliwa Kuwa Mchezaji Bora Novemba, Mgunda Kocha Bora

0

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Fiston Mayele amechaguliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba huku Kocha Juma Mgunda wa Simba akichaguliwa kuwa kocha bora.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi la Ligi Kuu Tanzania, imesema kikao cha kamati ya Tuzo za TFF kilichokutana jijini Dar es Salaam Jumanne ya Disemba 6, ndicho kilichowatangaza Mayele na Mgunda kuwa washindi.

 

Pia kamati hiyo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Liti uliopo mkoani Singida, Hassan Simba kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Novemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Leave A Reply