The House of Favourite Newspapers

Fiston Mayele Hauzwi… Yanga Waweka Masharti Magumu Kukaa Mezani Kuongea

0

UONGOZI wa Yanga umetamka kuwa mshambuliaji wao Mkongomani Fiston Mayele hayupo sokoni lakini wapo tayari kukaa meza moja kwa klabu zinazomuhitaji kwa ajili ya mazungumzo.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya mshambuliaji ambaye kinara wa mabao katika Kombe la Shirikisho Afrika mwenye mabao sawa sita na straika wa Marumo Gallants, Ranga Chivaviro kuwepo katika rada na baadhi ya klabu kubwa Afrika.

Kati ya klabu zinazotajwa kuwepo katika rada hizo za kumuwania mshambuliaji huyo kwa ajili ya msimu ujao ni Orland Pirates ya Afrika Kusini na US Berkane na Raja Casablanca zote za nchini Morocco.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa hakuna mchezaji yeyote aliyekuwepo katika hivi sasa aliyekuwepo sokoni akiwemo Mayele anayetajwa kuwaniwa na baadhi ya klabu kubwa Afrika.

Kamwe alisema kuwa kama uongozi haupo tayari kumuachia Mayele kutokana na staa huyo kuwepo katika mipango mikubwa ya kutengeneza timu itakayokuwa imara na tishio kimataifa katika msimu wakati wakienda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aliongeza kuwa kabla ya kuanza mazungumzo hayo ya Mayele na hizo klabu, kikubwa wafahamu kuwa dau la Mayele hivi sasa linafikia zaidi ya Sh 5Bil ambazo zitawashawishi wao wamuachie mshambuliaji huyo.

“Nimeona taarifa nyingi kuhusu kuwa yupo sokoni, wafahamu kabisa hizo klabu zinazomuhitaji kuwa Mayele ni mchezaji mwenye mkataba mkubwa wa kuichezea Yanga.

“Hivyo Mayele hayupo sokoni, lakini tupo tayari kufanya mazungumzo hizo klabu zilizoonyesha nia kubwa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wetu tegemeo.

“Kabla ya kuja lakini wakae wakifahamu kuwa dau lake ni zaidi ya Sh 5Bil, hatuwezi kuzuia mazungumzo ya klabu nyingine kikubwa taratibu zifuatwe,” alisema Kamwe.

STORI NA WILBERT MOLANDI

NI ZAIDI ya VITA! RAYVANNY na PAULA WATUPIANA MANENO MAZITO – “NAOMBA UNIACHE PIPILO”…

Leave A Reply