Kartra

Fiston: Nipo Fiti, Nisipofunga Nitatoa Asisti

MSHAMBULIA JImpya wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razack, amesema kuwa yupo fiti kuikabili Kengold FC leo na kama hatafunga basi atasababisha bao ‘asisti’.

 

Mrundi huyu ametua Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu, na mpaka sasa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na hajafanikiwa kuwakonga mashabiki wa timu hiyo kwani hajafunga wala kutoa asisti.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Fiston amesema kuwa: “Kama nitapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza au kama nikitokea benchi haina shida, lakini nimejiandaa kuhakikisha ninaisaidia timu yangu ipate matokeo mazuri.

 

“Kama sitaweza kufunga kwenye mechi hiyo basi nitajitahidi nisababishe upatikanaji wa bao ili timu ipate ushindi.”

STORI: CAREEN OSCAR,Dar es Salaam


Toa comment