Kartra

Fiston: Sitamani Kubaki Yanga, Naondoka

MSHAMBULIAJI wa Yanga FC, Fiston Abdoul Razack ameibuka na kusema kuwa hatamani kubaki tena ndani ya kikosi cha timu hiyo baada ya kocha Cedrik Kaze kuondoka.

 

Mrundi huyu aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu na kusaini kandarasi ya miezi sita, amefanikiwa kufunga mabao mawili tu, moja kwenye Ligi Kuu Bara na lingine katika Kombe la FA.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Fiston alisema kuwa: “Kwa sasa Yanga hawajanifuata kuhusu kuongeza mkataba na wala sitamani kuongeza tena mkataba.

“Najua kuwa wananchi walitamani kuona makubwa kutoka kwangu na mengi ila mimi kuna kitu nimekiona kwenye hii timu yaani wana tabia ya kuonjeshana (kukupa nafasi finyu uwanjani) tu hawawezi kumuacha mtu azoee.

 

Mtu asipofunga kipindi cha kwanza kipindi cha pili wanawaza kumtoa na usipofunga mechi moja basi mechi ijayo hupati nafasi ya kuanza.“Kama kocha Cedric Kaze angekuwepo basi ningefanya makubwa zaidi maana yule ananijua na anajua jinsi ya kunitumia.

STORI: CAREEN OSCAR, Dar es Salaam


Toa comment