Flavian Matata Anavyorudisha kwa Jamii!

 

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Bongo, Flaviana Matata ‘Flav’ anaendelea kuwa mfano wa mastaa wanaorudisha kwa jamii baada ya kuzindua bidhaa zake mpya za taulo za kike (pedi).

Flav amezipa taulo hizo jina la Lavy Sanitary Pads huku lengo kuu likiwa ni kusaidia wanafunzi hasa wasichana wasiokuwa na uwezo.

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Flav ambaye pia ni mjasiriamali amesema lengo la kuanzisha bidhaa hizo ni kutaka kusaidia watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kununua pedi wanapopata hedhi hali inayosababisha kukosa masomo.

STORI: MEMORISE RICHARD NA HAPPYNESS MASUNGA

 

Toa comment