FLAVIANA MATATA ATAENDELEA KUWA MATATA KWELI

Image result for FLAVIANA MATATA

FLAVIANA MATATA

UKIFIKA katika Jiji la Los Angeles, Marekani kuna eneo linaitwa West Sunset amb-alo ndani yake kuna kampuni moja kubwa ya mitindo inayoitwa The Lions, ukiuliza jina la Flaviana utaambiwa yule Matata kutoka Tanzania (Bongo)? Lakini pia ukienda Jiji la Paris nchini Ufaransa utakutana na kampuni nyingine kubwa ya mitindo ya Next Model Management na ukiulizia jina Flaviana utaambiwa tu yule mwanamitindo anayetokea Tanzania? Kama hiyo haitoshi, ukichanganya miguu yako kutalii kisha ukatua Barcelona, Hispania katika Kampuni ya Mitindo ya Sight Management Studio ukaulizia Flaviana jibu litakuwa lilelile!

Hata ukija Afrika ukitua Jiji la Johannesburg, moja kwa moja katika Kampuni ya Boss Models ukamuulizia Flaviana utashangaa wengine wakikujibu kwa lugha ya Kiswahili kabisa; Unamuulizia huyu wa kutoka Tanzania? Flaviana ni mmoja kati ya wanamitindo kutoka Tanzania wanaofanya vizuri nje ya nchi. Mwaka 2013, Jarida la Forbes la Africa liliandika kwamba ni miongoni mwa wanamitindo saba ambao wanaingiza kipato kikubwa Afrika.

Kama hiyo haitoshi, mwaka jana aliandikwa na mtandao maarufu duniani wa okay.com kuwa ni miongoni mwa wanawake 100, wenye ushawishi zaidi barani Afrika, lakini pia mwanadada huyu mwenye urembo wa kipekee amefanikiwa kupamba majarida mengi yakiwemo New African Woman, Essence, i-D Magazine, Wonderland, True Love, Glamour, Marie Clare, Bang, Flare, Dar Live, Instyle, Italian Vogue, Nu Woman, Wanted, You Inspire, Nylon Magazine, Glass Magazine, Arise Magazine, FA Japan, Dazed and Confuse Magazine, Grazia Magazine pamoja na L’Officiel Paris Magazine. Utaachaje sasa kumfuatilia Flaviana Matata?Image result for FLAVIANA MATATA WITH  WIZ KHALIFA

Kibongo-bongo, Flaviana mbali na mitindo ni mjasiriamali, anamiliki bidhaa zenye Lebo ya Lavy ambazo ni rangi za kupaka kucha za mikononi pamoja na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation inayofanya kazi za kijamii kuwahamasisha mabinti wadogo kuhusu elimu, kupambana na kuamini kupitia vipaji vyao.

Ukiacha na yote hayo, Flaviana Matata amekuwa ‘akiwashtua’ Wabongo wengi pindi akitokelezea na mastaa mbalimbali mitandaoni na katika makala haya yanaanika mastaa wa dunia ambao ameshawahi kushea nao ‘maphotos’.

USHER RAYM-OND

Julai 2011, Flaviana alipata mualiko na mkali huyu wa muziki wa R&B duniani kupitia taasisi yake binafsi ya Usher New Look Foundation yenye lengo la kuwasaidia watoto wenye shida kuanzia umri wa miaka 10 na kuendelea ambapo mbali na kutembelea taasisi hiyo alipata wasaa wa kukaa naye kuzungumza sambamba na kupiga picha.

PARIS HILTON

Miongoni mwa mastaa wanamitindo wakubwa duniani ni Paris Hilton. Flaviana alipata mualiko wa kuungana naye kwenye bonge moja la tamasha la mitindo lililojulikana kama Dennis Basso Spring New York Fashion Week ambapo aliongozana na wanamitindo wenzake wakiwemo Tori Praver, Nicky Hilton Rothschild na Rosemary Kokuhilwa.

SHAQUILLE O’NEAL

Mstaafu huyu wa mpira wa kikapu aliyeweka historia katika Ligi ya NBA ambaye kwa sasa amebaki kama mchambuzi naye ni mmojawapo aliyewahi kuuza nyago kwenye picha na Flaviana akiwa katika moja ya mchezo wa NBA All Star.

Image result for FLAVIANA MATATA WITH NICKI MINAJ

NICKI MINAJ

Nani asiyemjua rapa huyu wa kike duniani? Hivi karibuni rapa huyo amewashangaza Wabongo wengi baada ya kutokelezea akiwa kwenye ‘redcarpet’ na Flaviana. Wawili hao walikutana katika sherehe za utoaji Tuzo za FMAS kwa mwaka 2018. Wapo mastaa wengi waliowahi kutokelezea katika picha ya pamoja na Flaviana ambapo pengine hakuna Mbongo aliyewahi japo kupata ‘selfie’ nao.

Mastaa hao ni pamoja na Mhariri na Mwenyekiti wa Jarida la Forbes, Steve Forbes ambalo ni maarufu kwa kufuatilia maisha ya watu mbalimbali na kutoa takwimu tofauti zinazohusu fedha, ameshakutana na rapa Wiz Khalifa pamoja na staa wa R&B, Kelly Rowland katika tamasha la Coachella huko Marekani. Pia alishakutana na Rapa Busta Rhymes, Rais Donald Trump, staa wa Hollywood, Gabriel Union na wengine kibao.Image result for FLAVIANA MATATA WITH  WIZ KHALIFA

 

ANDREW CARLOS

Loading...

Toa comment