The House of Favourite Newspapers

Fleva Imerudi Kama Zamani!

0

MUZIKI wa Bongo Fleva ni muziki wa aina yake, kwani haujawahi kuchuja tangu ulipoanza kama ilivyo Taarab na Dansi ambazo kwa sasa zinajikongoja. Hiyo yote ni kutokana na jinsi unavyoboreshwa na wasanii na namna unavyopokelewa kwenye jamii.

 

Kwa miaka ya zamani kama ya 2000, tulizoea kuona wasanii wakitoka na albam mbalimbali za nyimbo zao. Albam hizo zilikuwa zikibeba nyimbo kadhaa. Baadhi ya wasanii waliotamba kwa kipindi hicho kwa kutoa albamu kali ni pamoja na; Juma Nature ambaye alitoa albam tatu; 2001 (Nini Chanzo), 2003 (Ugali) ambayo inasemekana kuwa albam ya kwanza kujaza ukumbi wa Diamond Jubilee kwa kipindi hicho.

 

Lady Jaydee alitoka na albam kama; Machozi mwaka 2000, Binti (2003) na Moto (2005).

Z Anto naye mwaka 2007 aliachia Binti Kiziwi, Profesa Jay, Ally Kiba, Chege, Temba na wengineo kibao nao walifanya hivyo.

Ghafla utaratibu wa kutoa albam ulitoweka hasa baada ya kuona ‘wanapigwa’ na mdosi mmoja aliyekuwa anasambaza.

 

Wakajikita zaidi kwenye singo na shoo. Wakawa wanaachia singo, wanafanya shoo ambazo ndizo zilizokuwa zinawaingizia kipato.

Wasanii wakasahau kabisa suala la kutoa albam. Msanii akitoa albam, anaonekana kama vile hajafikiri vizuri au amekosa washauri.

Ila kwenye miaka ya hivi karibuni hadi sasa, baadhi ya wasanii wameamua kuirudia Bongo Fleva ile ya zamani. Baadhi yao wameamua kutoa albam zilizobeba nyimbo zao kadhaa. Miongoni mwao ni:

 

DIAMOND

Machi 14, 2018, Diamond alikuja na album yake ya kwanza aliyoipa jina la A Boy From Tandale iliyo na jumla ya nyimbo 18.

 

Kwenye albam hiyo, ameweza kushirikiana na wasanii wakubwa kutoka nje kama Davido-Nigeria (Number One –Remix), Morgan Heritage (Hallelujah), Rick Ross (Waka), Miri Ben air (Baila), Omarion (African Beauty), Tiwa Savage (Fire), Ne-Yo (Marry You), Mr. Flavour (Nana), P- Square (Kidogo) na Jah Prayzah (Amanda). Albam yake ilifanya vizuri licha ya kuzinduliwa nchini Kenya, lakini ilihudhuriwa na watu wengi na kufana kinoma.

 

Kutoka kwa albam hii, kumeweza kuwahamasisha hata wasanii wa kizazi kipya na wao kutumia mfumo huo wa kutoa albam.

 

JUX

Ni mku rugenzi na mwa nzili shi wa brand ya mavazi ya African Boy. Licha ya kujiongeza kwenye biashara hiyo, pia Jux ni msanii mwenye mvuto kuanzia umbo hadi sauti na kusababisha kupendwa na wadada wengi.

 

Ni msanii wa miondoko ya RnB na The Love Album ni albamu yake ya kwanza aliyoitoa mwaka 2019 ikiwa na jumla ya nyimbo 18. Miongoni mwa nyimbo zinazopendwa sana kwenye albam hiyo ni pamoja na Sugua, Upofu, In Case You Don’t Know na nyinginezo.

 

VEE MONEY

Kati ya warembo wanaofanya poa kwenye anga la Bongo Fleva, Vee Money ni mmoja wapo. Kitaa luma ni mta nga zaji, lakini mnamo 2012 aliweza kuingia rasmi kwenye sanaa ya muziki ambapo Ommy Dimpoz alimshika mkono na kufanya naye ngoma kali iliyobamba kwa kipindi hicho, iliyokwenda kwa jina la Me and You.

 

Licha ya kuachia ngoma kali na nyingi, lakini mapema 2018 akaamua kuachia albam yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Money Mondays, iliyo na jumla ya nyimbo 18 huku akiwashirikisha mastaa mbalimbali kutoka nje ya nchi kama; Mohombi, Konshens, Cassper Nyovest pamoja na KO kwenye No Body But Me.

 

HARMONIZE

Baada ya kujiengua kwenye lebo iliyomkuza kisanii ya WCB iliyo chini ya msanii Diamond Platnumz, mapema mwaka huu akaamua kuachia albam yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Afro East.

Albam hiyo ina jumla ya nyimbo 18 zilizowaunganisha wakali kibao kutoka nje ya Bongo kama; Phyno (Body), Burna Boy (Your Body), Skales, Yemi Alade (Pain), Khaligraph Jones (Die) nakadhalika.

Ni albam iliyopokelewa vizuri na watu kutokana na nyimbo zake nyingi kuwa na mashairi mazuri.

 

LADY JAYDEE

Ni mkongwe wa muziki wa kizazi kipya asiyechuja tangu alipoingia rasmi kwenye gemu hilo miaka ya 2000. Amewavutia wasanii wengi wa kike hadi na wao kuingia kwenye gemu.

Licha ya kutoa albam kadhaa na kutikisa vilivyo, mwaka 2018 akaamua kuja na ujio wa albamu nyingine ya Woman iliyosheheni nyimbo 10, miongoni mwa zilizotamba ni pamoja na Ndi Ndi Ndi, Nasimama na Una tatizo Gani.

 

Mbali na wasanii hao, wasanii wengine wameamua kutoa (Extended Playlist) utambulisho wa nyimbo chache za albamu, ambao ni kama: Lulu Diva, Rayvanny nakadhalika. Hivyo kutokana na wasanii hao kutoa albam ambazo zilizoeleka kwa kipindi cha nyuma, ni dhahiri kuwa Bongo Fleva inarudi ilipotoka.

MAKALA: AMINA SAID

Leave A Reply