FLORA AFUNGUKA MBASHA KUTANUA NA BINTIYE

MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa kwenye muziki wa Injili Bongo, Flora Kusekwa ‘Madam Flora’ ameyafungukia yale madai mazito mno juu ya mtalaka wake, Emmanuel Mbasha kutanua hotelini na bintiye, Elizabeth Emmanuel. 

 

Kufuatia picha za Mbasha na bintiye wakila bata kama lote hotelini huko Zanzibar kusambaa mitandaoni, kuliibuka maneo mengi na sintofahamu ambayo hakuna aliyepata nafasi ya kusikia neno la Mbasha au Flora kama mama wa Eliza.

 

Gazeti hili la Risasi Jumamosi lilijipa jukumu la kumtafuta Mbasha, lakini lilipomkosa lilimgeukia Madam Flora ili azungumzie sababu ya kumuachia mtoto wake huyo wa kike kutanua na mzazi wake huyo wa kiume kila kona kiasi cha kuzua maswali kwa ‘wananzengo’ wanaofuatilia kwa karibu mambo ya mitandao ya kijamii.

 

HUYU HAPA  MADAM FLORA

Risasi Jumamosi: Kumekuwa na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na mtalaka wako (Emmanuel Mbasha) kuzunguka na mtoto wenu kwenye mahoteli makubwa, unazungumziaje hilo?

 

Madam Flora: Jamani kwa upande wangu mimi naona hakuna tatizo lolote kabisa. Yule ni baba yake hivyo watu wamuache mtoto ale raha kwa baba yake.

Risasi Jumamosi: Kwa nini sasa mtoto wa kike kama yule anaongozana na baba yake kila sehemu na wewe unakubali?

Madam Flora: Jamani yule ni baba yake, siyo kijana tu wa mtaani, sasa niwe na wasiwasi wa nini tena?

Risasi Jumamosi: Vipi ile ishu ya kuonekana yupo chumbani kwa mtoto maana ndiyo ilisemwa sana kwenye mitandao? Unaizungumziaje?

 

Madam Flora: Hivi jamani naomba kuuliza, huko mitaani baba zao au wazazi wao hawajawahi kuingia kwenye vyumba vya mabinti zao? Maana mimi naona ni kitu cha kawaida kabisa na ndiyo maana tangu awali nikasema angekuwa ni kijana mwingine ningeshtuka sana.

Risasi Jumamosi: Kwa hiyo sasa hivi mtoto hakai kwako?

Madam Flora: Yupo kwa baba yake anakula raha jamani, baadaye atakuja wala hakuna tatizo lolote, maana si unajua mtoto wa kike ni baba?

Risasi Jumamosi: Haya asante sana Madam Flora.

Madam Flora: Asante sana.

 

Flora na Mbasha ambao wote ni waimbaji wakubwa wa nyimbo za Injili walijaliwa mtoto huyo mmoja katika ndoa yao kabla ya kutalikiana ambapo mwanamama huyo aliolewa na mwanaume mwingine, lakini jamaa huyo mpaka sasa bado hajaoa.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi


Loading...

Toa comment