The House of Favourite Newspapers

Flyover ya Ubungo (Mwenge – Buguruni) Yaanza Kutumika – Pichaz

0
BARABARA za juu eneo la Ubungo Interchange upande wa Mwenge – Buguruni, jijini Dar es Salaam imeaanza kutumika rasmi baada y ujenzi wake kukamilika.

Barabara hizo zimeanza kutumika  rasmi leo Jumatano, Septemba 30, 2020, kwa magari kupita.

Ujenzi wa ‘Ubungo Interchange’ katika makutano ya Barabara za Nelson Mandela, Sam Nujoma na Morogoro unagharimu TZS 200.7B na utawezesha magari 65,000 yanayotumia barabara hizo kupita bila msongamano mkubwa.

Watumiaji wa barabara hiyo wameshindwa kujizuia na kuelezea shukrani zao kwa serikali  ya Rais Dkt. John Magufuli baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utakuwa mkombozi wa adha ya foleni kwa wakazi wa Dar.

Mradi huo ulikuwa ukiendeshwa na Kampuni ya Ujenzi ya China Civil Engineering and Construction Corporation (CCEC). 

Ujenzi wake ulizinduliwa Machi 20, 2017 baada ya Rais  Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuweka jiwe la msingi.

Shamra za ufunguzi huo zilifanyika leo majira ya asubuhi na kuhusisha wafanyakazi kadhaa wa mradi huo.

Sehemu ya chini ya mradi huo ilifunguliwa rasmi Mei 30,  na kutatua kikamilifu tatizo la msongamano na foleni zilizokuwa katika makutano ya barabara hizo.  Sehemu iliyobakia itakamilika mnamo miezi mitatu ijayo ambapo mradi mzima utakabidhiwa mwishoni mwa mwaka huu na kutoa fursa bora zaidi kwa watu wanaopita sehemu hiyo.

Leave A Reply