The House of Favourite Newspapers

Wajue Walioingiza Mkwanja Mrefu Zaidi Duniani 2018

 

JARIDA maarufu duniani la biashara la ‘Forbes’ limetoa orodha ya watu kumi maarufu walioingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2018.

 

Orodha hiyo imejumuisha watangazaji, wanariadha, wanamuziki, wacheza filamu na wafanya mazingaombwe.

 

Kilichoshika vichwa vya habari ni baada ya rapa Jay-Z kuingia kwenye orodha hiyo huku akigongana na mwanadada Kylie Jenner, wote wakiingiza kiasi cha Dola milioni 900.

 

Orodha kamili ni ifuatayo:

 

1.George Lucas  –  Dola bilioni 5.4

 

Ni mwaandaji wa filamu, mjasiriamali na ni mmiliki  wa kampuni ya Industrial Light, Magic na Lucasfilm.

Utajiri wake umenyanyuka baada ya kuiuza kampuni yake ya Lucasfilm mwaka 2012 kwa kampuni kubwa ya Disney mwaka 2012 na kuchukua kiasi cha Dola bilioni 4.1.

 

2.Steven Spielberg – Dola bilioni 3.7

 

Ni mwaandaji wa filamu.  Anaingiza mkwanja huo kupitia kampuni yake ya Dreamworks Animation na mradi wake wa Ready Player one ambao tayari una filamu yenye jina hilo na imeweza kupendwa na asilia zaidi ya 90 duniani kote.

 

3.Oprah Winfrey – Dola bilioni 2.8

 

Ni mmiliki wa vyombo vya habari, muigizaji, mtangazaji na mtayarishaji wa vipindi.  Kiwango kikubwa cha pesa yake kinaingizwa na uwekezaji wake kwenye kampuni yake ya Weight Watchers inayohusika na mambo ya afya.

 

4.Michael Jordan – Dola bilioni 1.7

 

Ni mchezaji mstaafu maarufu wa mpira wa kikapu.  Asilimia 90 ya pesa aliyoingiza ni kutokana na viatu vyake vya Jordan ambavyo vimemuingizia zaidi ya Dola milioni 800

 

5.Kylie Jenner – Dola milioni 900

 

Ni mtangazaji wa televishen, modo, mjasiriamali, staa wa instagram.  Ameweza kuingiza kiasi cha Dola zaidi ya milioni 630 toka amezindua kampuni yake ya vipodozi miaka miwili iliyopita.

 

6.Jay-Z – Dola milioni 900

 

Ni mwanamuziki, mjasiriamali, mwandishi wa muziki na ni mtengenezaji wa muziki.   Kiasi kikubwa cha pesa amekipata kutoka kwenye dili zake na kampuni ya shampeni ya Armand de Brignac na D’Ussé cognac ambazo zimemuingizia zaidi ya Dola milioni 90 kwa mwaka 2017.

 

7.David Copperfield – Dola milioni 875

 

Ni mtu mfanya mazingaombwe na ameshafanikiwa kutwaa tuzo 21 za Emmy kwa vipengele alivyokuwa akigombea 38.   Kiasi kikubwa cha pesa kinaingia kutokana na matamasha  katika kumbi na viwanja mbalimbali duniani.

 

8.Diddy – Dola milioni 825

 

Ni mwandishi, mwanamuziki, muigizaji, mjasiriamali, na ni mtengenezaji wa muziki.  Kiasi cha pesa zake kinaingia kutokana na nguo za Sean John, kinywaji cha Ciroc Vodka na kampuni yake ya Revolt TV  na DeLeón tequila.

 

9.Tiger Woods – Dola milioni 800 

 

Ni mchezaji maarufu wa mchezo wa golf na amekuwa mmoja miongoni mwa wachezaji wa juu wa kulipwa kwa muda wa miaka mingi.

Kiasi chake cha pesa kinaingia kutokana na malipo yake anayoyapata katika mchezo huo.

 

10.James Patterson – Dola milioni 800

 

Ni mwanafalsafa na mwandishi maarufu wa vitabu vya riwaya. Mauzo ya vitabu vyake yamemwezesha kukaa kwenye nafasi ya 10 kwenye watu maarufu duniani.

Comments are closed.