The House of Favourite Newspapers

Mayele, Moloko Waimaliza Azam – Video

0

FISTON Mayele na Jesus Moloko ambao wote ni raia wa DR Congo, jana waliimaliza Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.


Mayele na Moloko walifunga
mabao hayo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar kuanzia saa 1:00 usiku.

 

Katika mchezo huo ambao mastaa wa Yanga waliingia uwanjani wakiwa na furaha baada ya kuweka mambo sawa na mabosi zao juu ya bonasi za mechi zilizopita, Mayele alianza kuitanguliza timu yake kwa bao
la dakika ya 36 akimalizia pasi ya
Kibwana Shomary.

 

Kuingia kwa bao hilo, kuliifanya Yanga kuzidi kushambulia kwa kasi na kuiacha Azam ikipanga mashambulizi yake yasiyokuwa na matokeo chanya.


Katika kipindi cha kwanza
ambacho timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu, kilimalizika kwa Yanga kuwa
mbele kwa bao 1-0.

 

Kipindi cha pili, dakika ya 68, Moloko aliifungia Yanga bao la pili na kuihakikishia ushindi Yanga uliowapeleka kileleni zaidi baada ya kufikisha pointi 12.

 

Yanga ikiwa imecheza mechi Nabi atajwa Simbanne, imefanikiwa kuweka rekodi ya aina yake ikiwa haijaruhusu bao mpaka sasa, huku ikifunga mabao sita.

 

Awali Yanga ilianza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold, lakini sasa imeanza kuongeza mabao.Kabla ya mchezo wa jana, ilitoka kuifunga KMC mabao 2-0 na kuifanya sasa katika mechi mbili mfululizo imepata ushindi wa zaidi ya bao moja tofauti na awali.

WAANZA KUUOTA UBINGWA
Wakati ligi ikiwa bado
haijachanganya sana, Yanga wameanza kuuota ubingwa wa Ligi Kuu Bara kutokana na kasi
waliyoanza nayo ambayo hakuna
timu nyingine inayowaweza kwa sasa kirekodi.

 

Yanga ikiwa imeshinda mechi zake kwa asilimia mia moja, inafuatiwa na Dodoma Jiji yenye pointi kumi ikicheza tano, huku Polisi Tanzania yenye pointi tisa, ikishika nafasi ya tatu na mabingwa watetezi Simba ambao leo wanacheza dhidi ya Coastal Union, wapo nafasi ya tano kwa alama saba. Ya nne ni Kagera Sugar.

Baada ya mchezo wa jana, mashabiki wa Yanga waliokuwa Uwanja wa Mkapa, walisikika wakisema kwamba moto
huo waliokuwa nao timu yao,
hauzimwi mpaka mwisho wa msimu, hivyo ubingwa ni wao baada ya kuukosa kwa misimu minne ambao ulitua Simba.

Leave A Reply