The House of Favourite Newspapers

Fujo kwenye kampeni zamtia wasiwasi Maimartha

0

MAIMARTHA6.jpgGABRIEL NG’OSHA

MH! Mtangazaji mahiri wa runinga Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ amesema anahofia fujo zinazofanywa na baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa kwenye mikutano ya kampeni kwamba ni hatari na ni dalili za uvunjifu wa amani baada ya uchaguzi mkuu.

Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, Mai alitolea mfano wa baadhi ya wafuasi wa chama f’lani wanaokwenda kwenye mkutano wa chama kingine na kuanza kuonesha ishara au mbwembwe zao, kukashifu na mengine jambo ambalo si sahihi.

“Kwenda kwenye mkutano wa chama kingine na kuonesha ishara za chama pinzani, kufanya fujo, kuwapiga, kuzomea au namna yoyote ile ni uchokozi, ni dalili za uvunjifu wa amani zinazoweza kutokea hata baada ya uchaguzi mkuu, tufanye siasa za amani, na si ugomvi na matusi,” alisema Mai.

Leave A Reply