The House of Favourite Newspapers

Fulham Yafanikiwa Kupanda Daraja, Sasa Kucheza Ligi Kuu ya Uingereza Msimu Ujao

0
Mshambuliaji wa klabu ya Fulham Aleksandar Mitrovic amefunga jumla ya mabao 40

KLABU ya Fulham yenye makao yake jijini London katika Uwanja wa Craven Cottage imefanikiwa kupanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Uingereza EPL msimu ujao wa 2022/2023.

 

Klabu hiyo imefanikiwa kupanda daraja mara baada ya jana kuifunga klabu ya Preston kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo mabao mawili yalifungwa na mshambuliaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic aliyefunga mabao mawili huku bao jingine likifungwa na Fabio Carvalho raia wa Ureno ambaye msimu ujao atajiunga na Liverpool.

 

Katika harakati za kupanda daraja Fulham imefanikiwa kushinda michezo 26 kutoka sare michezo 8 na kupoteza michezo 8 huku klabu hiyo ikifikisha jumla ya pointi 98.

Mashabiki wa Fulham wakifurahi klabu yao kurejea Ligi Kuu nchini Uingereza

Kwa upande mwingine mshambuliaji hatari na tegemezi wa klabu hiyo Aleksandar Mitrovic amefikisha jumla ya mabao 40 ikiwa ni mabao mawili nyuma ya rekodi iliyowekwa na Guy Whittingham akiwa na Portsmouth kwenye msimu wa 1992-1993 alipofunga jumla ya mabao 42.

 

Naye kocha wa Fulham Marco Silva amesema klabu hiyo ilistahili kupanda daraja na kwamba ilikuwa na kila sababu ya kujivunia mafanikio iliyopata.

 

 

 

Leave A Reply