‘Full Dozi Concert’ Yatoa Burudani Aina Yake Dar Live

Msanii wa Bongo Fleva, Q Chilla au Q Chief, akifanya shoo ya aina yake ndani ya Ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live wakati wa tamasha la Full Dozi lililofanyika usiku wa kuamkia leo.

Msanii wa burudani Snura Mushi akifanya yaka stejini usiku wa kuamkia leo.

…Akiongea na mashabiki zake.

…’Mama Chura’ akifanya majonjo ambayo yamempa umaarufu mkubwa nchini ya kukata mauno.

Mwanamuziki Beka aliyekuwa Yamoto Bendi, akitoa burudani kali ndani ya Dar Live.

Juma Nature akiwasalimia mashabiki zake usiku za kuamkia leo.

…Akiimba na mashabiki.

TAMASHA  la Full Dozi lililoandaliwa na ITV, Redio One na Capital Redio ambalo  lilifanyika usiku wa kuamkia Jumapili ndani ya Ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live,  lilikuwa kivutio cha aina yake.

Katika burudani  hiyo wasanii mbalimbali waliojumuika,  walifanya vitu adimu kwa  mashabiki waliojaa ukumbini hapo na kuufanya uonekane mdogo.

Wasanii hao ni Snura Mushi, Nature, Sharo Mwamba, Beka Flavour, Q Chilla, Hamorapa  na bendi ya muziki wa dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Tamasha hilo limeacha gumzo kutokana na kukidhi haja ya mashabiki hao ambao mara kwa mara ‘waliwavamia’ wasanii kama Juma Nature,  Q Chilla, Beka Flevour na kuwatunza huku wakiwaomba kurudia nyimbo zao kila walipomaliza kutumbuiza.

Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo mashabiki wengi walitaka burudani kama hiyo ifanyike kila mwaka ili kutoa fursa ya aina hiyo kwa watu wengi zaidi.

Na Issa Mnally/GPL

Live: Gwajima Aliamsha Dude Kushambuliwa Kwa Tundu Lissu
Toa comment