The House of Favourite Newspapers

FULL TIME: TAIFA STARS 2-0 CAPE VERDE, KUFUZU AFCON

 

FULL TIME

Mchezo umemalizika, Taifa Stars inapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde.

Dk ya 95: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka Samatta anaingia Rashidi Mandawa.

Dk ya 93: Stars wanatengeneza shambulizi lakini shuti la Fei Toto linadakwa.

Dk ya 92: Cape Verde wanaongeza kasi ya kushambulia, wanafika langoni mwa Stars.

Zinaongezwa dakika 5 za nyongeza.

Dk ya 90: Stars wamepunguza kasi ya kushambulia, mashabiki wanaongeza kasi ya kushangilia wakiamini ushindi uko upande wao.

Dk ya 87: Msuva yupo chini kaumia, anapatiwa matibabu. Mchezo umesimama kwa muda.

Dk ya 84: Cape Verde wanapata kona, inapigwa Manula anadaka.

Dk ya 82: Samatta yupo chini, ameumia, watoa huduma wanaingia wanamtoa nje.

Dk ya 77: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Kumbuka katika mchezo uliopita baina ya timu hizo, Cape Verde wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Taifa Stars, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita.

Dk ya 74: Manula yupo chini baada ya kuumia wakati akiokoa mpira, mchezo umesimama kwa muda.

Dk ya 70: Mchezo ni mkali na timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dk ya 67: Taifa Stars wanafanya shambulizi kali lakini beki wa Cape Verde anafanya kazi nzuri kwa kuokoa krosi ya Samatta.

Dk ya 66: Cape Verde wanapata kona.

Dk ya 65: Himid Mao wa Stars anachezewa faulo, inapigwa kuelekea lango la Cape Verde.

Dk ya 64: Stars wanapata nafasi shuti linapaa juu ya lango.

Dk ya 60: Cape Verde wanapata faulo karibu na lango la Taifa Stars.

Dk ya 59: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka Mudathir anaingia Fei Toto,

Dk ya 58: Samatta anaipatia Taifa Stars bao la pilin kwa shuti kali akiunganisha pasi ya Mudathiri Yahaya.

Dk ya 58: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 53: Cape Verde wanapata mpira wa kurusha.

Dk ya 52: Abdi Banda ametoka, nafasi yake imechukuliwa na John Bocco.

Dk ya 50: Cape Verde wanapata kona, inapigwa inaokolewa na walinzi wa Stars

Dk ya 48: Mchezo umebalansi kwa timu zote kupeana zamu ya kumiliki.

Dk ya 46: Taifa Stars wanafika langoni mwa Cape Verde lakini wanakosa umakini.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia kuanza kwa kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Dk ya 45: Zinaongezwa dakika 2 za nyongeza. Cape Verde wanapata faulo, MManula anapangua mpira unakuwa wa kurushwa.

Dk ya 44: Cape Verde wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka inakuwa goal kick.

Dk ya 42: Mchezo umesimama kwa muda, kipa wa Stars, Aishi Manula anapatibwa matibabu ya mkono.

Dk ya 41: Mpira bado upo kwenye lango la Taifa Stars.

Dk ya 39: Kona inapigwa almanusura iingine, mpira unatoka unakuwa wa kurushwa kwenda kwa Stars.

Dk ya 39: Almanusura Shomari Kapombe ajifunge baada ya kupiga kichwa kinatoka nje, inakuwa kona.

Dk ya 38: Krosi nzuri ya Samatta inatua kwa Msuva anapiga shuti linatoka nje kidogo ya lango.

Dk ya 35: Mchezo umesimama kwa muda, mchezaji wa Stars yupo chini akipatiwa matibabu.

Dk ya 31: Mashabiki wa Tanzania wanaongeza kasi ya kushangilia.

Dk ya 29: Kazi nzuri ya Samatta inamfanya Msuva kumalizia kwa kufunga bao safi

Dk ya 29: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 27: Tanzania wanaendelea kujipanga taratibu.

Dk ya 26: Cape verde wanapata kona, inapigwa inaokolewa.

Dk ya 24: Timu zinaanza kupeana zamu kumiliki mpira.

Dk ya 22: Mbwana Samatta anakosa penati, mpira unagonga nguzo ya juu na kurejea uwanjani kisha walinzi wanaokoa.

Dk ya 21: Penatiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Tanzania wanapata penati, Msuva anachezewa faulo ndani ya eneo la 18.

Dk ya 20: Garry Rodrigues anapata kadi ya njani kwa kuonyesha nidhamu mbovu.

Dk ya 16: Cape Verde wanafanya shambulizi kali, shuti linapita karibu na lango.

Dk ya 15: Shambulizi lingine, Stars wanashindwa kujipanga vizuri.

Dk ya 13: Stars wanafanya shambulizi, Msuva anapata nafasi anapiga shuti linapaa juu ya lango.

Dk ya 10: Cape Verde wanapata kona, inapigwa inatoka nje inakuwa goal kick.

Dk ya 9: Tanzania wanajaribu kufanya shambulizi la kushtukiza lakini kasi ya Simon Msuva inakuwa ndogo.

Dk ya 6: Wageni Cape Verde wanapiga pasi kadhaa, nao wanaonyesha hawana kasi.

Dk ya 4: Taifa Stars bado wanapanga mashambulizi taratibu.

Dk ya 1: Kasi ya mchezo ni ndogo.

Mchezo umeshaanza

Huu ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2019, mchezo unapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.