FULL VIDEO: Usiku wa Tuzo za VPL 2017/18 Mlimani City

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco, ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Bocco ametwaa tuzo hiyo huku akiwapiku wachezaji wenzake beki Erasto Nyoni na Emmanuel Okwi ambao pia walikuwa kwenye kinyang’anyiro.

Ukiachana na tuzo ya mchezaji bora VPL, Bocco ambaye ni Nahodha wa kikosi cha Simba amekuwa na msimu mzuri kwa kufanikiwa kubeba pia tuzo ya Mo akiwa mchezaji bora ndani ya timu hiyo.

Toa comment