The House of Favourite Newspapers

FUNDI WELDING ASEMA ALIMUONA MBOWE AKIONGOZA MAANDAMANO MKWAJUNI

SHAHIDI kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upande  wa Jamhuri amesema kuwa alimuona Freeman Mbowe, Halima Mdee, John Mnyika na Ester Matiko wakiongoza maandamano katika eneo la Mkwajuni Aprili 16, 218.

Katika ushahidi wake amesema kuwa siku hiyo  alikuwa akitokea eneo analofanyika kazi la Mkwajuni kuelekea upande wa  pili wa barabara kufuatilia vifaa vya ufundi welding na ndiyo alishuhudia kundi la watu wakitokea eneo la Morocco kuelekea Magomeni huku wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwemo ‘Hatupoi’.

 

 

Kauli hiyo ameitoa wakati kesi ilipokuja katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba ambapo alikuwa akiongozwa na wakili wa serikali Paul Kadushi huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala.

 

 

Shahidi huyo amesema kuwa wakati akiwa katika duka alilokuwa akinunua vifaa kwa ajili ya ufundi welding aliona gari la polisi likipita huku likihamasisha kundi hilo kuondoka mara moja na ghafla ndipo mabomu ya machozi yalianza kurushwa na yeye kuamua kukimbia.

 

 

Katika kesi hiyo viongozi tisa wa Chadema akiwemo katibu mkuu wa chama hicho na viongozi wengine wanadaiwa kufanya mkusanyiko, na maandamano Februari 16,218 usiokuwa na kibali katika eneo la Mkwajuni  jijini  Dar es Salaam.

 

Comments are closed.