Fursa kwa Vijana: Kampuni ya Inalipa Yazindua Programu ya Uza Kukuza Ujasiriamali
Kampuni ya biashara mtandaoni ya Inalipa (https://www.inalipainc.com) leo imezindua programu mpya ya kibunifu ya uza ambayo inatazamiwa kuwa chombo kinachohitajika sana kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.
Inalipa ni kampuni maarufu ya biashara mtandaoni iliyopo nchini Tanzania ambayo imefanikiwa kupata sifa toka pande zote Afrika kwa dhamira yake kujenga mfumo mpya na bora kufikia soko la bidhaa mbalimbali ndani ya Africa. Inalipa ni moja ya kampuni chache za kitanzania zilizoweza kuvutia uwekezaji wa kimataifa kutoka kampuni maarufu za uwekezaji wa ubia unaolenga kampuni zenye muelekeo chanya kiteknolojia.
Dira ya msingi ya inalipa ni kuona Afrika ambayo kampuni kubwa za bidhaa za walaji zinapata urahisi wa kusambaza bidhaa katika soko, kupata taarifa muhimu ambazo zitawasaidia kuwa na ufahamu mzuri wa wateja wao.
Inalipa inaamini wauzaji wa kati, wauzaji wadogo na maduka ni wadau muhimu katika maendeleo ya sekta ya rejareja.
Leo inalipa imezindua uza, ambayo ni programu (app) ya mauzo ambayo inaruhusu mtu yeyote kujiunga na kuwa bosi binafsi kwa kuuza bidhaa kwa jumla. Uza ni bidhaa yenye mfumo wa kusisimua ambao unatoa zawadi za papo hapo kwa watumiaji wake, ina ubao utakaoonyesha msimamo wa wanaoongoza wenye ushindani kwa wauzaji kupata zawadi na zaidi.
“Tunaamini katika nguvu ya vijana kuendesha maendeleo ya Tanzania na kutuongoza kwa siku za usoni. Tuna vijana milioni moja wanaohitimu na kuingia katika soko la ajira kila mwaka. Vijana hawa wana uwezo wa ujasiriamali ila hawana usaidizi unaofaa kujipatia kipato. Uza ni jibu letu katika hili na tunaamini italeta mapinduzi katika sekta” amesema Hafiz Juma, CEO wa inalipa.
Inalipa inaongeza uza katika kundi la bidhaa zao ambazo ni pamoja na inalipa JUMLA ambayo ni programu (app) inayohusika na mauzo ya bidhaa za jumla na inalipa ambayo ni programu (app) ya biashara ya mtandaoni ya bidhaa za rejareja kwa walaji.
Kwa ubunifu wa makampuni kama inalipa, kuna uelekeo mzuri wa mustakabali wa siku za usoni kwa vijana wa Tanzania.