#GlobalCelebrities: Future Azungumzia Uhusiano Wake Na Ciara Kwa Sasa, Uongozi Wa Donald Trump & Mengine.

Baada ya kuachana na aliyekuwa girlfriend wake wakati huo Ciara, Future amefanya interview na jarida la Billboard Magazine na kufunguka baadhi ya mambo kuhusiana na uhusiano wake na mwanamuzikia na mama huyo.

Nimetembelea mtandao wa Billboard na huko nimekutana na interview aliyoifanya Future Hendrix na jarida la Billboard na kuzungumzia vitu vingi ikiwemo album yake mpya, maisha yake ya sasa na ex-girlfriend na baby mama wa mtoto wake Ciara.

Hivi ni baadhi ya vitu alivyoongea na Billboard:

Kuhusu uhusiano wake na Ciara na jinsi anavyumudu kwa sasa:

Nahisi kama kila kitu kilitokea kwa mipango na kusudi za Mungu. Nina furaha na maisha yangu sasa hivi, licha ya kuwa mimi na yeye tulishamalizana…. niko poa na wala sihitaji kujihusisha na mahusiano yatakayo ondoa furaha yangu ya maisha. Najua nina uwezo wa kuwa mtu bora, sijajikatia tamaa bado, kwahiyo ukikataa tamaa juu yangu sina chochote cha ziada cha kukuambia. Kwani ukikataa tamaa juu ya kitu ambacho kilikuwa real, basi ina maana mahusiano hayo hayakuwa real kwako. ” 

Anauonaje uongozi mpya wa Rais Donald Trump:

Sihitaji kujihushisha na hayo mambo, sijui kama unanisoma vizuri? Na wala sihitaji hilo jina litajwe tajwe kwenye interview yangu. Huko ni kuzinguana…

Kuisoma interview nzima ya Future, tembelea Billboard.com.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Picha: Billboard.com.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.


Loading...

Toa comment