G NAKO: AMENIPA MTOTO, NAMZAWADIA NDOA !

George Sixtus Mdemu ‘G Nako’ na mpenzi wake Yasinta

MKALI wa Bongo Fleva kutoka Kundi la Weusi, George Sixtus Mdemu ‘G Nako’ amesema kuwa, baada ya mpenzi wake aitwaye Yasinta kumpatia mtoto wa pili ambaye ni wa kike aliyempa jina la Gianna atampa zawadi ya ndoa.  Akipiga stori na Over Ze Weekend, G Nako alisema kuwa, ana furaha Mwenyezi Mungu kumjalia mtoto huyo na kutokana na furaha hiyo atampa mama wa watoto wake zawadi ya kudumu ambayo ni ndoa.

“Nimefurahi sana! Nina mtoto wa kike ambaye kwa sasa ana miaka kumi lakini kumpata na huyu wa pili wa kike ndio furaha imeongezeka zaidi, namshukuru mama Gianna na namuahidi zawadi ya ndoa soon,” alisema G Nako. G Nako kwa sasa anatamba na Ngoma ya Weka ambayo anatarajia kuitolea video ili kuzikonga nyoyo za mashabiki wake.


Loading...

Toa comment