GABONI: CAF Wamfanyia Vipimo Serengeti Boy Aliyeichapa Angola Iwapo Anatumia Dawa

GABON: Winga teleza wa Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka mchezaji bora wa mechi ya Serengeti Boys na Angola hapo jana, alichukuliwa na maafisaa wa CAF kufanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli.

Hali hiyo ilisababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora hivyo akawakilishwa na mlinzi, Dickson Job. CAF hawakuamini walichokiona kwa Abdul ambaye alihaha uwanja mzima!

Hata hivyo baada ya vipimo ilibainika hakuwa katumia dawa hizo bali ni uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani.

#GabonMpakaKombelaDunia


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment