Gadiel Michael Atoa Ujumbe Mzito Kwa Mashabiki Yanga

Gadiel Michael

BAADA ya Klabu ya Simba, kumtambulisha beki mpya wa kushoto,  Julai 9, 2019,  Gadiel Michael,  kwa kumpa mkataba wa miaka miwili, mchezaji huyo leo amewaambia mashabiki wa Yanga, kupitia mtandao wa Instagram, kwamba soka ndiyo msingi wa maisha yake na kwamba mwisho wa yote maisha yake atayabeba mwenyewe.

Kupitia page yake ya Instagram,  amewaomba radhi mashabiki wa Yanga akiandika:

”Wakati mwingine mtu unalazimika kufanya maamuzi yako peke yko kwa sababu anaewajibika na maisha yko mwisho wa siku ni mtu mwenyewe… Mpira ndio kazi yangu ya kimaisha, maamuzi niliyoyafanya yalikuwa ni muhimu sasa kwa maslai yangu na familia yangu… Nimuombe rathi aliekuwa meneja wangu Jemedari saidi kazumari kutokana na sintofahamu iliuotokea kwa kutomshirikisha nikiamini asingekubali nihame mtaa. Nimelazimika kufanya maamuzi magumu kwa maslai mapana yangu mwenyewe na familia yangu… Kikubwa ni kwamba Mpira ni familia moja, bado tuko kwenye familia, HAKUNA CHUKI, MAISHA YAENDELEE… Niwashukuru wanaYanga wote kwa ushirikiano walioniptia, nilikuwa na furaha san kwao. Pia niwashukuru viongozi wa Yanga chini ya mzee Msolla. Mm ni mwanadamu, kiumbe dhaifu, Maana aliekamilika ni mola wetu pekee. Nawaomba rathi sana. Asante🙏

Loading...

Toa comment