Gadner, Jide Mambo Ni Moto

AMKENI amkeni kumekucha, unaambiwa ile kapo mashuhuri Bongo ya Mtangazaji Gadner G. Habash na Malkia wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’, imeamka upya na kuzua gumzo kama lote!

 

Wawili hawa kabla ya kumwagana miaka kadhaa iliyopita na kila mtu kuishi maisha yake, walikuwa wanandoa waliodumu kwa muda mrefu kabla ya kuachana kwa talaka mahakamani.

 

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na wawili hao, vimeeleza kuwa, siku za hivi karibuni wawili hao wamekuwa wakijiachia pamoja kuashiria huenda wakawa wamemaliza tofauti zao na kuamua kuishi vizuri kama mke na mume.

 

“Kuna kila dalili kwamba mambo ni mazuri sana kwa wawili hawa maana si unakumbuka walikuwa kama chui na paka, lakini sasa hivi mambo ni moto, wanajiachia pamoja,” kilieleza moja ya chanzo makini.

 

Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, mbali na kuonekana pamoja, hata mitandaoni wamekuwa wakipostiana kuashiria kwamba hakuna tena bifu kati yao.

 

“Wewe fuatilia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii hususan Instagram, utaona kila mmoja anamposti mwenzake tena akisindikiza na ujumbe mzuri tu,” kilisema chanzo hicho.

 

AMANI liliperuzi kwenye ukurasa wa Instagram wa Gadner na kukutana na posti ambayo inaonesha wawili hao hivi karibuni walikuwa pamoja kwenye moja ya fukwe za Zanzibar.

 

Gadner aliposti picha ya Jide akiwa kwenye boti akiwa na bosi kubwa wa Clouds Media Group; Joseph Kusaga na kusindikiza na meneno mawili tu:

“Zanzibar pazuri.”

 

Baada ya kuandika maneno hayo, komenti zilikuwa kama zote kwenye picha hiyo ambapo watu wengi waliwapongeza wakiamini wapo pamoja na sasa mambo ni bambam.

 

Jitihada za kuwapata wawili hao ili waweze kuzungumzia maisha yao mapya ya sasa, ziligonga mwamba kufuatia kupigiwa simu na kutopokea.

Stori: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Toa comment