The House of Favourite Newspapers

Gairo wamtaka Shabiby tu

0

IMG_0402Mgombea ubunge wa jimbo la Gairo mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hemed Shabiby akihutubia wananchi.

Mwandishi wetu, Gairo

WAPIGAKURA wa Jimbo la Gairo mkoani Morogoro wamesema bado wana imani na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hemed Shabiby.

Wakizungumza na Wikienda katika moja ya kampeni za mgombea huyo jimboni humo juzi, wapigakura hao walisema kutokana na mbunge huyo aliyemaliza muda wake kuleta maendeleo jimboni humo, hawaoni sababu ya kuchagua mwingine.

gairo“Ndugu mwandishi nadhani hoja kubwa ya jimbo hili ni nani awe rais, lakini kwenye ishu ya ubunge liko wazi, ni Shabiby tu,” alisema mpigakura mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Masua.

“Zamani tulikuwa na tabu ya zahanati, Shabiby ametuletea, madaktari wapo mpaka wa upasuaji. Maji yapo, na nimeona mradi wa maji unaendelea hata vijijini. Hakuna mwanafunzi anayekaa chini eti uhaba wa madawati. Sasa tunamtaka nani?” alihoji mpiga kura mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Msafiri ‘Mlibya’.

Mbunge huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mabasi ya Shabiby Line yanayofanya safari zake kati ya Dar na baadhi ya mikoa, anatajwa kuleta maendeleo makubwa katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita.

Miongoni mwa mambo makubwa aliyofanya ni upatikanaji wa maji jimboni, tatizo ambalo kwa kipindi kirefu lilikuwa likiwasumbua. Wakulima kupata matrekta ambayo wanayatumia kwa kilimo, kujengwa kwa Kituo cha Afya cha Gairo ambacho kina chumba cha upasuaji, barabara zinazopitika majira yote na kuboresha elimu.

Wikienda lilizungumza na Shabiby mwenyewe ambapo alisema:

“Nimeamua kugombea tena kwa sababu wananchi wa Gairo wananihitaji. Mafanikio makubwa niliyowaletea yamewafurahisha.

“Nawaomba wananchi wa Gairo wanipe tena nafasi kwa sababu kama kawaida yangu, mimi si mtu wa maneno mengi bali vitendo.”

Leave A Reply