Gallas kumbadili Coulibaly Simba

BEKI wa kulia Simba, Zana Coulibaly huenda msimu huu ukawa wa mwisho ndani ya kikosi hicho baada ya uongozi kuwa katika harakati za kumsajili William Lucian ‘Gallas’ ili aje kuchukua nafasi yake.

 

Lakini pia inadaiwa wako kwenye mazungumza na Haruna Shamte wa Lipuli ambaye ni kiraka. Inadaiwa kuwa uongozi huo wa Simba upo katika mazungumzo na mchezaji huyo Gallas ambaye pia amewahi kuitumikia timu hiyo kabla ya kwenda Ndanda FC na baadaye Lipuli.

 

Sababu ya kutaka kuachana na Coulibaly ni kutokana na kutovutiwa na kiwango chake ambacho amekuwa akikionyesha katika mechi za hivi karibuni.

Loading...

Toa comment