GAME 1: Golden Warriors Waichapa Cleveland Cavaliers 124-114
SHUGHULI ya fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) imeanza baada ya Golden State Warriors kuiliza Cleveland Cavaliers 124-114 kwenye mechi ya kwanza usiku wa kuamkia jana Ijumaa.
Mechi hiyo ilikuwa kali huku kipindi cha kwanza kikisisimua zaidi, ambapo timu zote mbili zilikuwa zinajaribu kufunga pointi kwa mitupo ya mbali.
Kipindi cha pili kilikuwa kikali zaidi, ambapo Golden S t a t e w a l i s h a m b u l i a v i k a l i h u k u C a v a l i e r s wakilazimika kuzuia presha hiyo kali.
Mc h ezo huo u l i i n g i a dosari katika dakika za mwisho baada ya staa wa Cavaliers Tristan T h omp s o m kutolewa na mwamuzi, ambapo wachezaji wa pande zote walizongana kutaka kupigana.
Pamoja na LeBron James kuifungia Cavavlier pointi 51 na kutoa asisti nane bado hazikusaidia timu hiyo kuibuka na ushindi.
Staa wa Warriors, Steph Curry alifungia timu yake pointi 29 wakati Draymond Green aliongeza pointi 13 na kutoa asisti tisa.
Timu hizo zitavaana kwenye mechi ya tatu ya fainali ya ligi NBA keshokutwa Jumatatu.
Warriors itaikaribisha Cavaliers kwenye uwanja wao wa Oracle Arena ambapo itawania kushinda tena ili kuongeza matumaini yao ya kutetea taji lao.
Comments are closed.