GARDNER AFUNGUKA KURUDIANA NA JIDE

Mtangazaji wa Radio Clouds FM, Gardner G. Habbash ‘Kapteini’ akiwa na aliyekuwa mke wake mwanamuziki mahiri wa kike wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’.

SIKU zote kuna usemi usemao penzi la kweli halifi! Hivyo ndivyo inavyoonekana kwa ‘maselebriti’ wawili wa Bongo, Mtangazaji wa Radio Clouds FM, Gardner G. Habbash ‘Kapteini’ na mwanamuziki mahiri wa kike wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’ ambapo jamaa huyo amelazimika kufunguka juu ya kurudiana kwao.

 

NI MIAKA MITANO SASA

Takriban miaka mitano sasa tangu mwaka 2014 walipotengana kwa talaka, bado Gardner anadaiwa kuwa na ‘homa’ ya kushindwa kabisa kumsahau Jide aliyedumu naye kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10.

 

SIRI YAFICHUKA

Siri hiyo imefichuka siku chache baa ya mtangazaji huyo mahiri kuposti picha ya kitambo kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanamuziki huyo nchini Kenya kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kisima. Katika tuzo hizo za miaka hiyo, Jide alitwaa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Afrika Mashariki.

BAADA YA PICHA SASA

Baada ya Gardner kuposti picha hiyo ndipo wakaibuka watu wa karibu wa jamaa huyo wakithibitisha kwamba bado Jide hajamtoka jamaa huyo kwenye hisia zake na kwamba anammisi kinoma. Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao wakubwa nchini walikwenda mbali zaidi na kuhisi kuwa huenda wawili hao wapo njiani kurudiana. Wengine waliwaomba chondechonde warudiane kwani ni miongoni mwa ‘kapo’ bora kabisa kuwahi kutokea Bongo na kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

Kufuatia hisia hizo, Gazeti la Ijumaa lilijipa ‘asainmenti’ ya kumtafuta Gardner ili kung’amua kinachohisiwa na mashabiki ndipo akafunguka juu ya ishu ya kurudiana kwao.

HUYU HAPA GARDNER

Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa katikati ya wiki hii, Gardner alianza kwa kuzungumzia picha hiyo aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram ambayo ndiyo chanzo cha kuzuka kwa maswali lukuki. Gardner aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa anashangaa kwa nini watu waliona ni kitu cha ajabu kwa sababu ni ukweli ulio wazi kwamba hajawahi kuacha kumkumbuka wala hajawahi kumsahau mtalaka wake huyo.

“Labda niseme wazi kwamba mimi sijawahi sijawahi kumsahau Lady Jaydee, ndiyo maana mtu akiniambia nimemkumbuka, nashangaa kwa sababu mtu unayemkumbuka ni yule uliyemsahau. “Lakini kwangu yeye (Jide) sijamsahau hata kidogo, yupo tu siku zote kwenye akili yangu,” alisema Gardner anayeendesha Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

DALILI ZA KURUDIANA?

Alipoulizwa kama kuposti picha huko kunaashiria dalili za kurudiana na kurejesha ndoa yao upya, Gardner alicheka mno na kusema alifurahishwa na jambo hilo, lakini kwa sasa angeomba liachwe hivyohivyo. “Hilo la kurudiana? Kwa kweli naomba tuliache kwanza, tuliache hivyohivyo tu,” alisema Gardner huku akiangua kicheko cha kufa mtu!

GARDNER NA JIDE

Gardner na Jide walifunga ndoa Mei 14, 2005, lakini hawakubarikiwa kupata mtoto. Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka Agosti, 2014.

Baada ya hapo, mwaka 2016, Jide alimtambulisha mpenzi wake mpya wa kumrithi Gardner ambaye ni mwanamuziki aitwaye Spice, raia wa Nigeria, lakini kwa upande wa Gardner hajawahi kumtambulisha mrithi rasmi wa Jide zaidi ya tetesi za hapa na pale ambazo huwa hazithibitishwi.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Toa comment