GARETH BALE AKARIBIA KUONDOKA REAL MADRID

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale anakaribia kuondoka katika klabu hiyo kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Zinedine Zidane. Mchezaji huyo wa taifa la Wales aliwachwa nje wakati Real Madrid ilipolazwa 3-1 na Bayern Munich nchini Marekani. Akizungumza baada ya mechi hiyo, Zidane alisema: Tunatumai ataondoka karibuni. Itakuwa vyema kwa kila mmoja wetu.

Tunaandaa uhamisho wake kwa timu nyengine. Sina ubinfasi wowote dhidi yake , lakini inafikia wakati ambao lazima mambo yafanyike. Bale ambaye ana miaka mitatu iliosalia katika kandarasi yake ameshinda kombe la mabingwa Ulaya mara nne tangu uhamisho wake wa £85m kujiunga na Madrid kutokaTottenham mwaka 2013 – ambapo ulivunja rekodi ya dunia mwaka huo.

Akijibu matamshi ya Zidane ajenti wa Bale Jonathan Barnetta aliambia AFP: Zidane ni aibu hana heshima kwa mchezaji ambaye ameifanyia makubwa Real Madrid. Majeraha yamerudisha nyuma harakati za mchezaji huyo wa Wales akiichezea Real Madrid mara 79 pekee katika misimu minne. Alicheza mechi 42 msimu uliopita nusu ya mechi hizo akiwa mchezaji wa ziada.

Bale alizomwa na mashabiki wa nyumbani msimu uliokwisha , ijapokuwa ajenti wake alisema mnamo mwezi Machi kwamba mchezaji huyo alitaka kumaliza kipindi chake cha mchezo katika uwanja wa Bernabeu.

”Lazima tufanya uamuzi lazima tubadilishe”, aliongezea Zidane. ”Uamuzi wa kuondoka ni wa Mkufunzi na mchezaji ambaye anaelewa hali ilivyo. Hali itabadilika sijui baada ya saa 24 ama 48, lakini itabadilika, na ni vyema kwa kila mtu”. Bale alikuwa mchezaji wa ziada msimu uliopita huku Real ikikamilisha kampeni yake mbaya zaidi nyumbani katika kipindi cha miaka 20, ikishinda mara 12 kujipatia pointi 68 na kumaliza katika nafasi ya tatu alama 19 nyuma ya mabingwa wa ligi Barcelona.

Pia walibanduliwa katika kombe la mabingwa na Ajax katika hatua ya muondoano. Zidane alirudi katika uwanja wa Bernabeu mnamo mwezi Machi na kuwa kocha wa tatu wa klabu hiyo msimu huu.

Wakati huo Barnett aliambia BBC kwamba usajili wa Zidane ulikuwa habari mbaya kwa kuwa hakupenda kufanya kazi na Bale na kwamba wawili hao wametofautiana kuhusu mbinu ya mchezo. Siku ya Jumapili Barnett aliambia BBC Wales kwamba tunafanya mambo fulani. ”Gareth Bale ni mchezaji wa Real Madrid lakini iwapo atakubali kuondoka utakuwa uamuzi wake mwenyewe, sio wa Zidane”.

Mbali na mataji manne ya ligi ya mabingwa, Bale ameshinda taji la la Liga , Copa del Ray na mataji matatu ya Uefa mbali na lile la klabu bingwa duniani akiichezea Real Madrid. Amewafungia mabingwa hao wa Uhispania zaidi ya magoli 100 lakini amepewa jina la utani la The Golfer na wachezaji wenzake na kipa wa Real Thibaut Courtois pia alisema kwamba Bale alikosa chakula chake cha jioni kwa kuwa hakutaka kukosa kulala wakati wake wa kawaida.


Loading...

Toa comment