Gari la Kubebea Wagonjwa Lakamatwa na Mirungi

Gari la kubebea wagonjwa (ambulance) la Hospitali ya Wilaya ya Tarime lenye namba za DFPA 2955 limekamatwa likiwa  na kilo 800 za madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Mkuu wa Polisi Mkoa  (RPC) wa Mara,  Juma Ndaki,  amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili. Gari hilo lilikuwa linatoka Mwanza kwenda Tarime.

“Tumewakamata na mirungi kilo 800 na tunawashikilia watu wawili.  Gari lilikuwa linatoka Mwanza kwenda Tarime, hivyo ushauri wangu ni lazima tuwe makini tunapoajiri madereva serikalini,” alisema kamanda huyo.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment