The House of Favourite Newspapers

Gari lamwaga mafuta ya mawese , lasababisha utelezi barabarani Dar

0

1.Baadhi ya vijana wakioneka wakiondoa mafuta barabarani yaliyomwangika.

Vijana wakiondoa mafuta yaliyomwagika barabarani.

2.Mwonekano wa eneo hilo.

Mwonekano wa eneo hilo.

4.Zoezi likiendelea la uchotaji maji.

 Usafishaji wa barabara kwa maji ukiendelea.

5.Mfereji ukionekana kujaa mafuta yaliyomwangika.

Mfereji uliojaa mafuta yaliyomwangika.

6. Kibao cha angalizo cha kupunguza mwendo kwa madereva.

Ilani inayowajulisha madereva utelezi uliokuwa mbele.

GARI lililokuwa na mafuta ya mawese jana usiku lilikwanguliwa na gari jingine wakati limeegesha kando ya Barabara ya Nyerere eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam na kusababisha kufunguka kwa loki za matenki ya mafuta hayo na kuyafanya yamwagike katika eneo kubwa la barabara karibu na kituo cha reli cha Tazara.

Tukio hilo lilisababisha utelezi katika barabara hiyo ambapo ungeweza kuleta ajali kwa magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo.

Katika kukabili tatizo hilo wahusika walihakikisha utelezi huo unaondolewa kwa kusafishwa kwa maji kama kamera ya mtandao huu ilivyofika eneo hilo leo.

HABAR/PICHA: NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply