Gari ya Diamond cha Mtoto
TANGU headlines za Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kukunua ndinga mpya aina ya Escalade kumekuwa na kelele nyingi mitandaoni.
Watu wake karibu siku hizi wanaitwa machawa, wamekuwa wakivuka mipaka na kuiita gari hiyo kama ndege ya chini na kwamba eti ni miongoni mwa magari ya gharama kubwa duniani.
Tupa kando akili hizo za kitoto; gari ya Diamond ni cha mtoto ile mbaya kwenye ulimwengu wa magari ya kifahari na yenye gharama kubwa, ila Kibongobongo; aaaah dole.
Hizi hapa ni aina kumi za gari za kifahari duniani pamoja na bei zake kwa mwaka huu 2021.
MOJA- Bugatti La Voiture Noire (dola 12.5Mil) sawa na shilini Bil 28.9.
PILI -Bugatti Centodieci(dola 9Mil) sawa na shilingi 20.8Bil.
TATU-Bugatti Divo (dola 5.7Mil) sawa na shilingi 13.2Bil.
NNE- Pagani Huayra (dola 3.7Mil) sawa na shilingi 8.5Bil.
TANO-McLaren Sabre(dola 3.5Mil) sawa na shilingi 8.1Bil.
Sita Aston Martin Valkyrie,
SABA-Bugatti Chiron,
NANE- Koenigsegg Jesko
Mercedes-AMG One ndizo zinafunga kumi bora ya mwaka.
Hata kama utasogeza namba hadi 20 aina ya gari la Diamond hutakutana nayo maana haipo kwenye top 20 ya magari makali na ghali zaidi duniani.