The House of Favourite Newspapers

GAUNI LAMTOA NISHAI UWOYA

SIKU chache baada ya staa wa sinema za Kibongo, lrene Uwoya kuingia kwenye sekeseke la kuwatupia pesa waandishi wa habari na kuzua mjadala mzito, wikiendi iliyopita yalimsibu makubwa baada ya gauni alilovaa kumtoa nishai.  Ilikuwa usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita kwenye Shindano la Miss Morogoro 2019 lililofanyika katika bustani ya Hoteli ya Morogoro ambapo Uwoya alikuwa mmoja wa majaji. Uwoya alipigwa chabo na gazeti hili akishindwa kutembea kutokana na gauni  alilovaa lililoacha sehemu kubwa ya ule upaja wake nje na kusababisha wanaume ‘kuvimba’ macho kwa kumtamani.

Hata hivyo, katika hali ya nishai Uwoya alilikanyaga gauni hilo likataka kumpeleka chini akiwa stejini ambapo shukurani zimwendee mwanamitindo Martin Kadinda ambaye alimwokoa kupiga mwereka mbele ya kadamnasi la sivyo mambo yote yangekuwa hadharani laivu bila chenga.

“Kwani hilo gauni amelazimishwa kuvaa? Ona sasa hawezi kufanya lolote mapaja yote nje na hata kukaa au kutembea yenyewe ni shida,” alisika mmoja wa wadau waliohudhuria shughuli hiyo. Katika shindano hilo, mtangazaji wa Clouds FM, Mussa Hussein alikuwa mmoja wa ma-MC ambapo alitumia nafasi hiyo kujibu mapigo kwa Uwoya ambaye aliamua kusimamisha shughuli hiyo na kulipa kisasi kwa kummwagia Uwoya pesa ambaye alizipokea kwa shingo upande.

Hata hivyo, mara baada ya kupokea pesa hizo za noti za elfu mojamoja Uwoya alimuita Mussa na kuteta naye huku akimuoneshea kidole kama cha shari hivi. Mwandishi wetu hakuweza kung’amua mara moja ni kitu gani walichoteta.

Baada ya wawili hao kumaliza kuteta, mwandishi wetu alimfuata Mussa ambapo alipotakiwa kuelezea tukio hilo alijibu; “Unakumbuka juzikati Uwoya akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari alifanya tukio la kuwatupia pesa waandishi wa habari ambao baadhi yao walidaiwa kugombea pesa hizo.

“Hivyo na mimi leo baada ya kubahatika kumuona Uwoya, nikiwa kama mwanahabari niliamua kujibu mapigo kwa kummwagia pesa ili ajue siyo wasanii tu wenye pesa bali hata waandishi pia tuna pesa za kuchezea.” Kwa upande wa burudani iliporomoshwa na Christian Bella na Malaika Band huku bendera ya Bongo Fleva ikipeperushwa vyema na Dully Skykes

Comments are closed.