Gavana Joshua Dariye wa Nigeria Afungwa Miaka 14 kwa Ubadhirifu

Seneta Joshua Dariye akiwa mahakamani.

Seneta Joshua Dariye  wa Jimbo la Plateau Magharibi, Nigeria, amepatikana na hatia na kufungwa jela kwa ubadhirifu wa  Naira bilioni 1.162 alipokuwa gavana wa jimbo hilo kati ya mwaka 1999 na 2007.

Dariye, ambaye alitiwa hatiani kwanza mwaka  2007 kwa makosa 23 yanayotokana na  kosa hilo, alitiwa hatiani tena na Mahakama Kuu ya Shirikisho chini ya Jaji Adebukola Banjoko, kwenda jela miaka miwili kwa kuvunja uaminifu,  na miaka 14 kwa ubadhirifu wa fedha hizo.

Mwanasheria wa Dariye, Paul Erokoro,  alisema mteja wake “hakuelewa kosa hilo” wakati linafanyika.

…Akiwa analia mahakamani.

Mwanseheria huyo alidai mteja wake “alikuwa akiwindwa na utawala wa kijeshi kwa miaka mingi, hivyo hakujua chochote kuhusu ufisadi wa fedha na mambo mengine yenye kuhusiana na jambo hilo.”

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment