The House of Favourite Newspapers

Gavana wa Benki Kuu Uingereza Atetea Ongezeko la Viwango vya Fedha

0
Andrew Bailey, Gavana wa Benki Kuu ya Uingereza

GAVANA wa Benki kuu ya Uingereza Andrew Bailey, ametetea uamuzi wake wa kuongeza viwango vya riba, Viwango vya riba vilipanda hadi 1.75 kwa kipindi cha miaka 27 iliyopita.

 

Kwa sasa Uingereza inatarajia kukumbwa na mfumko wa bei unaotarajiwa kugonga zaidi ya 13% kwa mwaka huu.

 

Uingereza inatabiriwa kuanguka katika mdororo wa uchumi, Mwaka huu utakaoshuka zaidi tangu mwaka 2008 ulipotabiriwa.

 

Kuongezeka kwa viwango vya riba ni njia mojawapo ya njia ya kujaribu kuthibiti mfumko wa bei kwani huongeza gharama za kukopa.

Gavana Bailey amesema kuna uwezekano wa riba kupanda hadi 13%

Hata hivyo kaya nyingi zatabanwa zaidi kufuatia kupanda kwa kiwango cha riba, kaya hizo ni Pamoja na zile zenye mikopo ya Nyumba.

 

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Suella Braverman amesema kuwa viwango vya riba vinapaswa kupandishwa.

 

Gavana wa hiyo Benki kuu ya Uingereza alinukuliwa leo wakati akiongea na BBC Radio 4

Gavana Bailey ameonya juu ya ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi kuwa linaweza kusababisha mfumuko mkubwa wa bei

“Hatari halisi tunayokabiliana nayo sasa ni mfumko wa bei unaoingia ndani na haushuki kwa njia ambayo tungetarajia, tumekuwa na mshtuko wa nyumbani pia tumekuwa na upungufu wa nguvu kazi katika kipindi cha miaka miwili hivi iliyopita”

 

Pia Gavana huyo ameonya dhidi ya nyongeza ya mishahara, akisema hii itafanya mfumko wa bei kuwa mbaya zaidi akaongezea kusema kuwa mfumko wa bei ukiongezeka zaidi Watu ambao wana hali ya chini ya kiuchumi ndio wataathirika zaidi kwa sababu hawana uwezo wa kujadiliana.

Leave A Reply