The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Betika kuingia mtaani kwa kishindo Jumatano hii

JUMATANO ya wiki hii Februari 13, 2019 inatarajiwa kuwa siku ya kwanza ya toleo la kwanza la Gazeti la Betika kuingia mtaani.

Gazeti hilo pekee nchini ambalo litakuwa linakuhabarisha kuhusiana na michezo na burudani linatarajiwa kuwa kivutio cha wahusika mbalimbali wanaoshiriki michezo ya kubashiri matokeo na ile ya bahati nasibu.

Akizungumzia ujio wa gazeti hilo, Kezilahabi Peresi ambaye ni Ofisa Masoko wa Gazeti la Betika, alisema ndani ya gazeti hilo wasomaji watapata makala kali za burudani na michezo bila kusahau hadithi kali ya kusisimua.

“Zaidi ya habari na uchambuzi wa mechi mbalimbali za ligi za nje, gazeti hili litakuwa linakuletea matangazo mbalimbali kutoka katika kampuni zinazoendesha michezo ya kubahatisha.

“Ndani ya Betika, utapata taarifa zote kuhusu kubeti na mbinu utakazoweza kutumia kubeti na kushinda.
“Wachambuzi wetu wa ndani na nje ya nchi tulionao watakusaidia kupata mwelekeo mzuri wa mechi zitakazochezwa katika wiki husika ili kukusaidia kufanya uchaguzi mzuri wa timu utakazobeti.

“Sisi Betika tunaamini, gazeti letu ni fursa nzuri kwa wabetiji wote kuelewa kwa undani kuhusiana na michezo ya kubahatisha, mambo ya kuzingatia ili kubeti kwa mafanikio na kuvuna pesa kwa wingi.

“Mbali na habari na uchambuzi wa michezo na burudani, tutakuletea taarifa za watu waliotajirika duniani kupitia michezo ya kubahatisha,” alisema Peresi na kuongeza:

“Aidha, tumetenga sehemu maalumu kwa ajili ya kuweka mikeka ya kubeti kutoka katika kampuni mbalimbali. Ni imani yetu Betika litakusaidia kuwa mbetiji wa faida badala ya kuwa msindikizaji.

“Sisi Betika ni tofauti na magazeti mengine, gazeti letu haliuzwi; utalipata bure kabisa. Kwa msingi huo, ukikutana na gazeti hili mahali popote, usikubali kutoa fedha yako, utatakiwa kuchukua bure.

“Timu nzima ya Betika tuna wahakikishia tumejipanga vilivyo kukuhabarisha na kukupa mbinu za kuwa mbetiji bora, lakini milango ipo wazi kutoa maoni yako kwa lengo la kuboresha zaidi.

“Hatutasita kupokea maoni na kuyafanyia kazi, yale yaliyo bora na yenye tija. Jione sehemu ya Betika kwa kututumia maoni yako kupitia mawasiliano yetu yaliyomo ndani ya gazeti hilo.

“Karibuni sana Betika, kupata maujuzi ya kuvuna mahela.”

Comments are closed.