The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Betika lapokewa Mbeya kwa shangwe

WASOMAJI wa Gazeti la Betika mkoani Mbeya wameuomba uongozi wa gazeti hilo kuweza kutoa mara kwa mara na kwa wingi ili kunufaika na utoaji wa matangazo yanayotolewa.

 

Maoni hayo yalitolewa wakati baadhi ya wauzaji wa magazeti walipokuwa wakigawa kwa wateja maeneo ya Mwanjelwa, Mafiati jijini Mbeya.

Mmoja wa wasomaji hao, Amos Juma alisema gazeti hilo limekuwa ni tofauti na dhana iliyopo ndani ya vichwa vya wasomaji wakidhani kuwa linahusu michezo ya kubahatisha wakati ndani kuna habari mbalimbali za kimichezo.

 

Alisema ndani ya gazeti hilo ameweza kupata habari za kimichezo pamoja na matangazo mbalimbali ambayo ni fursa kubwa kwa Watanzania kulitumia gazeti katika kutangaza matangazo ya bidhaa zao na matangazo tofautitofauti.

Msomaji mwingine, Hamis Mwakalasya alisema gezeti hilo limekuwa la kitofauti kutokana na kutolewa bure wakati magazeti mengi yamekuwa yakiuzwa na hakuna fursa ya kuweza kutoa matangazo kama yanayotolewa kwenye Gazeti la Betika.

 

“Hapa zimetolewa tu gazeti chache lakini mwitikio wa wasomaji ni mkubwa sana kiasi ambacho kila muda tukiwa tunalipata itakuwa ni rahisi kuweza kunufaika na fursa ya kutangaza matangazo yetu mbalimbali ya kibiashara,” alisisitiza Mwakalasya.

Alisema ndani ya gazeti hilo ameweza kupata habari mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za michezo ya kubahatisha ambapo msomaji anaweza kujifunza jinsi anavyoweza kujipatia bahati nasibu.

 

Naye, Mhariri wa Gazeti la Betika, John Joseph alipolizwa juu ya kazi yake hiyo alisema: “Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Wanaohitaji kutangaza nasi kwa kuwa gazeti letu asilimia kubwa limesheheni matangazo, tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au kupitia barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, mhusika anaweza kufika Sinza Mori kwenye jengo letu la Global Group.”

 

Aliongeza kuwa kwa watangazaji wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao mingine ya kijamii inayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers kwenye Istagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Comments are closed.