The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Betika Yatikisa Mwanza

0

MARA baada ya Gazeti la Betika kuingia mtaani Jumatano ya wiki hii lilitikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwemo Makoroboi, Kirumba, Buzuruga, Mkuyuni pamoja na Mabatini.

Gazeti hilo la bure ambalo utolewa kwa wasomaji wenye umri kuanzia miaka 18, lilisifiwa na wakazi wengi wa Mwanza huku kikubwa wakifurahia elimu na dondoo kuhudu kubeti ambavyo vyote vinapatikana ndani ya Betika.

Timu ya masoko ya Global Publishers ambao ndiyo wachapishaji wa gazeti hilo, ilitembelea maeneo mbalimbali na kugawa bure gazeti hilo, wasomaji wakawa wanapongeza ubunifu wa gazeti wakieleza ni wa kipekee nchini Tanzania.

Mmoja wa wasomaji aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Julius mkazi wa Mkuyuni, alisema amekuwa akilifuatilia na limemsaidia kushinda mikeka yake baada ya kupata dondoo za mechi mbalimbali.

Naye Feisal Richard wa Buzuruga alisema: “Nawapongeza Global, gazeti hili linatusaidia kwenye mikeka, unajua kubeti siku hizi ni kama kazi zingine.

“Mimi natumia hii kazi ya kubeti kwa sasa kulisha familia yangu na kupata nauli za watoto wangu kwenda shule, hivyo Gazeti la Betika limesaidia kuniongezea maarifa zaidi ya kubeti.”

Naye, Mhariri wa Gazeti la Betika, John Joseph alipolizwa juu ya kazi yake hiyo alisema: “Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Wanaohitaji kutangaza nasi kwa kuwa gazeti letu asilimia kubwa limesheheni matangazo, tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au kupitia barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, mhusika anaweza kufika Sinza Mori kwenye jengo letu la Global Group.”

Aliongeza kuwa kwa watangazaji wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao mingine ya kijamii inayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers kwenye Istagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Na Johnson James, Mwanza

 

Leave A Reply