The House of Favourite Newspapers

Gazeti la Spoti Xtra Lapokelewa Kwa Shangwe Mitaani

GAZETI jipya la michezo la Spoti Xtra linatolewa na Kampuni ya Global Group, jana toleo lake la kwanza lilipokelewa kwa shangwe kubwa iliyotokana na promosheni ya kuzunguka viunga mbalimbali vya Jiji la Dar.

Katika promotion hiyo, msafara wa wafanyakazi na wanenguaji waliokuwa wakisindikizwa na burudani ya muziki ulianza mapema asubuhi katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori kisha kuelekea Mwenge, Ubungo, Mabibo, Manzese, Kinondoni, Mwananyamala, Makumbusho, Kawe, Tegeta na kumalizia Soko la Tegeta-Nyuki ambapo wapenzi wa magazeti ya michezo walikuwa walikusanyika sehemu lilipokuwa likipatikana Gazeti la Spoti Xtra na kujinyakulia nakala zao.

Gazeti hilo lililonekana kubamba mitaani ambapo wasomaji wa magazeti waliohojiwa, hawakusita kuusifia muonekano wa ndani na nje wa gazeti hilo.

 

Muuza magazeti Na Richard Bukos, Dar kwenye Kituo cha Kawe aitwaye Juma alionesha furaha yake waziwazi kwa kushangilia ujio wa Spoti Xtra lililosheheni habari za burudani na michezo, hadithi za kusisimua kutoka kwa watunzi mahiri na uchambuzi wa michezo

Comments are closed.