The House of Favourite Newspapers

GAZETI LA SPOTI XTRA LAZIDI KUJIPANUA NCHINI

Ofisa Usambazaji  Keffa Massaga (kushoto) na muuzaji  magazeti ya Spoti Xtra, Lilian Richard (kulia mwenye T-Shirt nyeupe) wakimpa maelekezo mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo katika moja ya viunga vya Jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Wakazi wa Bunju  jijini Dar es Salaam wakilisoma Spoti Xtra kwa hamu kubwa.
Mfanyabiashara ya matunda wa Bunju A akiburudika na Spoti Xtra wakati akisubiri wateja.
Mkazi wa Bunju B jijini Dar akionyesha mshangao kufuatia habari motomoto na za kuvutia alizokutana nazo kwenye Spoti Xtra.
Muuza magazeti ya Spoti Xtra, Lilian Richard, akimpa zawadi ya sabuni mmoja wa wasomaji wa Bunju kwa kununua gazeti hilo.
Lilian Richard akimuuzia gazeti mmoja wa wasomaji wa Bunju A leo.

GAZETI la michezo la Spoti Xtra linalotolewa na Global Publishers Ltd, leo limeendelea kujipanua nchini kote ambapo wasomaji wengi wanajitokeza kulinunua na kulisoma ili kujiburudisha na stori na makala zake mbalimbali kuhusu michezo nchini na nchi za nje.

Pamoja na kulisambaa sehemu mbalimbali za nchini, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, waliendelea kulifurahia na kuonyesha furaha yao kwa kulisoma, hususan maeneo ya Bunju, Boko na Tegeta.

Spoti Xtra ni kila kitu katika michezo na burudani.

(PICHA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.