Geita Gold Yaipania Yanga

FELIX Minziro, Kocha msaidizi wa Geita Gold amebainisha kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu mbele ya Yanga Katika mchezo wa ligi utakaochezwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Huu ni mchezo wa pili kwa Geita Gold kucheza katika ligi kuu baada ya mchezo wao wa kwanza kupoteza kwa kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC.

 

Minziro amelieleza Championi Jumamosi kuwa: “Tumejipanga vizuri kuelekea mchezo dhidi ya Yanga na tupo tayari kucheza nao pia hatuwaogopi ila tunawaheshimu wapinzani wetu, niwaombe tu mashabiki watarajie mchezo mzuri hapo kesho (leo).

 

“Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza imetuumiza hivyo nguvu zetu ni kweye mchezo wetu dhidi ya Yanga, kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu, makosa yetu tumeyafanyia kazi.”

 

Aidha, Nahodha wa Geita Gold, Jofrey Manyasi alisema kuwa wachezaji wamekubaliana kuwapa furaha mashabiki wao.

WAANDISHI WETU, Dar es Salaam

4229
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment