Geita Gold Yashusha Mghana, Yapania Kufanya Makubwa Mashindano ya Shirikisho

Shawn Oduro

KLABU ya Geita Gold imetangaza kumsajili mlinzi Shawn Oduro raia wa Ghana kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni katika jitihada za kukifanyia marekebisho kikosi hicho kwa ajili ya mikiki mikiki ya ligi kuu na mashindano ya CAF.

 

Huu ni usajili wa nne wa wachimba madini hao baada ya George Wawa kutoka Dodoma Jiji, Hussein Kazi (Polisi TZ) na Mlinda mlango Arakaza MacAthur kutoka Burundi.

Beki raia wa Ghana amesajiliwa na Geita Gold FC

Nyota huyo ambaye anakuwa usajili wa pili wa Kimataifa ametua klabuni hapo kuziba pengo lililoachwa na Mkongwe Juma Nyosso aliyetimkia Ihefu ya Jijini Mbeya.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment